Sunday, October 21, 2012

Diamond Acharuka Asema'Epukeni Accont hii "Diamond Platnumz Swaqq" ya Facebook ni Fake"



"Ki ukweli nimevumilia sana hii tabia ila naona kama uzalendo umenishinda...mara kwa mara nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa wadau wangu mbalimbali kuwa nawajibu vibaya kwenye account yangu ya Facebook,Kucomment maneno machafu,Ku_upload picha chafu,Kuomba vocha,Kuomba pesa kwa njia ya Western union, M-pesa,Tigo Pesa na kadharika...


Kiukweli jambo hilo limekua likinisikitisha sana...hususan kupitia katika account hiyo chini yenye jina la "Diamond Platnumz Swaqq" pamoja na Account zingine nyingi zenye majina na picha zangu.... hivyo ningependa kuchkua fulsa hii kuwajuza Mashabiki na wadau wangu kua Account hiyo yenye jina la "Diamond Platnumz Swaqq" si ya kwangu ni ya mtu Fake ambae anatumia jina na picha zangu kuwachezea akili zenu....

Pili ningependa kukukaribisha rasmi katika Fan Page yangu iliyopo pembeni mwa Blogsite hii,uiLIKE page hiyo ili uweze kuungana na mimi na kuwa mtu wa kwanza kupata taarifa,kazi na matukio yangu yote ya kila siku kwa haraka zaidi..."

 Says Diamond

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...