Wednesday, October 10, 2012

FIESTA 2012: AIBU ZOOOTE, YA DIAMOND KIBOKO


Diamond na vijana wake wakivua nguo jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2012.
...Wakizidi kuonyesha nguo zao za ndani.
Diamond akiwa stejini.
INAWEZEKANA kwamba Tamasha la Fiesta 2012, lilikumbwa na matukio mengi ya aibu lakini lile la mwanamuziki Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’, kuvua nguo na kumwaga ‘lazi’ mbele ya maelfu ya Watanzania, likawa la funga kazi kuliko yote.


Diamond ambaye alishangiliwa vilivyo, wakati akitumbuiza na kudhihirisha kwamba yeye bado moto wa kuotea mbali anapokabidhiwa jukwaa, alipozidiwa na mzuka, alisaula suruali yake na kubakiwa na kivazi cha ndani ambacho wengi hukiita ‘boxer’ (chupi)...

Rick Ross akishusha burudani katika Fiesta 2012.
Mwanamuziki huyo, hakufanya hivyo peke yake, kwani aliposaula na wacheza shoo wake walimfanya vivyo hivyo, nao wakabakiwa na vi-boxer  vyao.
Warembo wakipagawa na shoo ya Rick Ross 'The Boss'.
Hawakuishia hapo, baada ya kuvua na kubaki hivyo, wakawapa migongo mashabiki na kuwachezea, hivyo kukamilisha zoezi la kumwaga ‘lazi’.


BABY MADAHA NAYE
Uchunguzi unaonesha kwamba mwanamuziki Baby  Madaha alikuwa msanii aliyetumia muda mwingi kujiandaa na shoo ya Fiesta 2012. Hata hivyo, jukwaa lilimkataa kutokana na mpangilio wa ratiba, kwa hiyo akabaki amejikunyata ‘back-stage’ wakati wasanii wenzake wakipanda jukwaani na kufanya kazi zao.

Baby Madaha akiwa katika pozi na jamaa.
Kwa upande mwingine, wasanii wa kiume walimuona kama ‘kiburudisho’ chao, kwani walipojisikia, walimvaa, wakamkumbatia na kumpiga mabusu.
Madaha katika pozi na Shetta.
Hili la kumkumbatia na kumpiga mabusu, lilichukuliwa kama ni la  kumfariji lakini wengine hususan wanamuziki wa kiume, walisema wanaona burudani kumkumbatia na kumbusu....


KUNA WAREMBO WALITWANGANA
Gari aina ya Mercedes Benz, lililombeba mwanamuziki wa Kimarekani, Rick Ross, lilipoingia uwanjani, warembo wawili walijikuta wakiwashiana moto, kila mmoja akimsema mwenzake kuwa ana kiherehere.



Warembo hao, kila mmoja alikuwa anataka kulishika gari hilo kwa lengo la kumfikia Rick Ross ‘The Boss’ lakini katika kile ambacho wengi walikiona ni cha ghafla, wao kwa wao walishikana.
Hata hivyo, warembo hao waliamuliwa na kuondolewa uwanjani hapo, hivyo kuambulia sifuri, kwani siyo tu kwamba walishindwa kumfikia mwanamuziki huyo, bali pia hata shoo yake hawakuiona.



TATHMINI YA JUMLA
Fiesta 2012, limekuwa na mafanikio zaidi kutokana na kumshusha nchini msanii ambaye anakubalika zaidi ulimwenguni kwa kipindi hiki. Rick Ross, yupo kwenye orodha ya wanamuziki wa Hip Hop daraja la kwanza kwa sasa ndiyo maana ujio wake, umeweza kuongeza chachandu ya aina yake kwenye Fiesta. Lingine ni kwamba Diamond aliweza kuwavalisha nguo wanamuziki wake wa safu ya kuimba, kwani kabla hawajapanda, walionekana wakiwa hawana jipya.
Wanamuziki wa Hip Hop, waling’ara vizuri kwenye Fiesta ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...