Tuesday, October 9, 2012

MAISHA: TUMIA MUDA WAKO KUJITATHMINI


Wengi wetu tumekuwa hatuna utamaduni wa kutenga muda wetu kwa ajili ya kujitathmini. Ili tufikie yale tunayotarajia kuyafikia katika safari yetu ya maendeleo kwanza kabisa ni lazima tujitathmini kwa mambo yafuatayo:-

1. UWEZO/STRENGTH TULIONAO

    Katika kujitathmini angalia unatumiaje uwezo wako katika kufikia malengo yako, wengi wetu hatuoni thamani ya uwezotulionao.Jipime unatumiaje uwezo wako wa KIELIMU kufikia malengo yako? mfano wa mambo yalio ndani ya uwezo wetu elimu, ujasiri,kujiamini, kuthubutu nk

  

2.UDHAIFU/WEAKNESS TULIONAO
 Hapa ni lazima tuangalie tunamadhaifu gani yanayokwamisha maendeleo yetu?msiku zote UDHAIFU ni hali tunazoruhusu wenyewe zitokee na tuna uwezo wa kudhibiti madhaifu tulonayo, katika kujitathmini angalia je udhaifu wako unakwamishaje malengo yako na kwa nini? baada ya hapo chukua hatua kuuudhiti udhaifu ulionao. mf wa udhaifu KUTOZINGATIA MUDA inakwamishaje safari ya maendeleo yako?

3.FURSA/OPPORTUNITY TULIZONAZO
katika fursa ni lazima ujitathmini je unafursa ngapi zinazoruhusu mianya ya maendeleo na kwa nini hutmii fursa ulizo nazo? tuzingatie kuna tofauti kati ya UWEZO na FURSA, uwezo ni mambo postive lakini yapoi nje ya uwezo wako, na fursa ni vitu postive lakini haviko ndani ya uwezo wako aidha vinatokana na jamii ilokuzunguka serkari nk. Mfano wa fursa labda uko ndani ya eneo zuri lenye rutuba je unatumiaje ardhi hiyo kufikia maendeleo yako

4.VITISHO/THREATS VINAVYOTUZUNGUKA
Katika hili ili kujitathmini ni lazima ujue vitisho juu ya jambo unalotaka kulifanya ni vipi? na namna gali utakabili vitisho hivyo??????

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...