Sunday, October 14, 2012

"TUNALAZIMIKA KUPIGWA NUSU UCHI ILI TUKABILIANE NA UGUMU WA MAISHA YA CHUO"....DENTI



Mmomonyoko wa maadili katika vyuo vikuu  hapa nchini umekuwa ukisababishwa na ugumu wa maisha  na kucheleweshwa  kwa hela ya kujikimu toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu hapa nchni na uongozi mbovu wa vyuo........

Wakiongea kwa nyakati tofauti na mtandao huu, baadhi ya wanafunzi hao toka vyuo mbalimbali wamedai kuwa maisha ya chuo ni magumu sana hasa kwa mtoto wa kike ambaye anahitaji vitu vingi ili aweze kujikimu kimaisha.......
"Kwa kweli maisha ya chuo ni magumu sana hasa kwetu sisi wasichana.Hela yetu ya kujikimu huchelewa sana.Wazazi nyumbani wanajua kuwa  tuna mkopo na wengine wanaimani finyu kuwa tunalipwa na serikali.......

Ukiomba hela nyumbani unagombezwa na hupewi au  wakikuonea huruma watakurushia  30,000  .Sasa hiyo hela inatosha kula, kununua mafuta,kusuka na vitu vingine?".......

Katika hali kama hii, inakuwa ni vigumu sana kwa mtoto wa kike kuvishinda vishawishi......Na ndipo  tunapolazima kutafuta sehemu ya kujihifadhi kwa wakaka......" Alieleza binti mmoja ambaye hivi sasa ni mwaka wa pili ( chuo tunakihifadhi)

Mbali na maoni hayo, mwanafunzi mwingine toka ukanda wa pwani alikuwa na mtazamo tofauti:

"Tatizo ni malezi ya kila mtu. Chuo na mapenzi havina uhusiano wowote.Mbona hata hata huko mtaani mapenzi yapo? Kwa nini wasilaumiwe wao?  Suala la msingi ni kwamba siku hizi uzushi mwingi.

Wanaume  wanatembea na simu zenye kamera. Ukilala  anakupiga picha alafu mkiachana anakuweka facebook."

Maoni ya huyu binti yalimfanya mwandishi wetu atake kujua zaidi  juu ya asili ya picha hizo za utupu maana zimekuwa zikipigwa katika pozi na si  kwa kuviziwa....

"Ni kweli baadhi yetu hufanya hivyo.Sasa hayo nimakubaliano yao.Pengine kaambiwa kwa kufanya hivyo atapewa hela ndefu zaidi na ukizingatia mfukoni hana kitu na  boom halitabiliki.Unadhani atafanyaje? .....

Kwa asilimia kubwa wasichana tupo katika wakati mgumu sana.Hata sisi hatupendi kupigwa tukiwa uchi ila  tunalazimika kutokana na mazingira"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...