Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nasarawa, Nigeria, Cynthia Osokogu (24) aliondoka Abuja mwishoni mwa mwezi Julai 2012 kwenda Lagos kununua nguo katika harakati zake za kibiashara
Cynthia alikuwa aki-chat na “Facebook friends” wapya aliofahamiana nao kupitia facebook hivi karibuni. Baada ya miezi kadhaa kupita, Cynthia urafiki ulikua na alifikia kuwaamini vijana hao, haswa kwa sababu nao walikua ni wanafunzi. Vijana hao walimuahidi Cynthia kwamba watampatia mahali pa kukaa atakapoenda Lagos katika harakati zake za biashara ya nguo.
Habari ambazo hazijathibitishwa na haijulikani kama zina ukweli wowote, zimesema kwamba vijana hao walimnunulia msichana huyo tiketi ya ndege, na pia kuahidi kumlipia chumba cha hoteli. Cynthia aliwaamini marafiki zake wapya, na hakujua kuwa walikua na mipango mibaya.
Vijana hao wawili walifika na kumpokea Cynthia kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos, na kumpeleka katika hoteli aliyofikia inayoitwa Festac. Walipofika katika hoteli, walimfunga kamba, wakampora fedha zake zote, na kumnyonga mpaka kufa.
kisha wakaondoka hotelini hapo haraka wakamfuta Cynthia kutoka katika orodha ya facebook friends wao kuondoa na kuondoa connection zote walizokua nazo na binti huyo.
Wafanyakazi wa hoteli waliukuta mwili wake na sababu kitambulisho chake na simu yake ya mkononi pia viliibiwa, polisi hawakuweza kumtambua hivyo kushindwa kuwatambulisha marafiki na familia yake. (Cha kujifunza: Ukisafiri kwenda mbali, hakikisha ndugu na jamaa wanajua hoteli uliyofikia, namba ya simu, na anuani ya hoteli hiyo)
Mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika jiji la Lagos. Muda wote huu, familia yake na marafiki, walikuwa wamekusanyika kumtafuta na walikua wakiomba kwa Mungu arudi salama.
Jinsi wauaji walivyokamatwa
Wakati wakiwa katika harakati za kumpra na kumuua Cynthia, mmoja wa wauaji hao alijibu simu ya Cynthia accidentally, na kampuni ya simu ilipoombwa kufuatilia simu ilipokelewa kutoka eneo gani, waligundua sehemu hiyo kuwa ni hoteli ya Festac. Jambo hilo liliwezesha familia ya marehemu kuwasiliana na hoteli na polisi wa eneo hilo, na hatimaye kupata mwili wa binti yao.
Kitu kingine, security camera (CCTV) ya hoteli hiyo, iliwarekodi wauaji hao na kusaidia kuwabainisha. Kulingana na taarifa, vijana hao wanafunzi wa chuo kikuu walipohojiwa, walikiri kumpora na kumuua Cynthia, na kusema kwamba binti huyo alikua ni mauaji yao ya sita!
Kundi la vijana hao limeripotiwa kuwa lime-specialize katika kuwalaghai wasichana, na baadae kuwapora kabla ya kuwaua. Ingawa kuna uvumi kwamba walikua wanafanya hivyo kama tambiko, inaonekana kwamba ilikuwa ni tamaa tu na lengo lao kuu ilikuwa kuwaibia na kuwaua.
Nini tunaweza kujifunza kutokana na hili
Dhahama kama hii inaweza kumtokea mtu yoyote. Katika social media, kama facebook, unaweza kuzoeana na mtu na kusababisha faraja bandia na zinazoweza kukupotosha na kuamini watu. Tunajua wanandoa ambao walikutana kupitia facebook au vikundi vya BBM na bado wako pamoja. Ukiwauliza kama walichukua hatua zozote za kuhakikisha usalama wao walipokutana mara ya kwanza, wengi watakiri kwamba hawakuchukua hatua zozote. Utasikia tu “urafiki wetu ulijengwa katika Twitter na BBM,” “Mara ya kwanza tulikutana kwenye nyumba ya mmoja wa marafiki. Ukweli ni chochote kinaweza kutokea. Kuwa makini na busara.
Cynthia alikuwa ni binti pekee wa wazazi wake – Meja Jenerali mstaafu Frank na Bi Joy Osokogu. Alikuwa akipendwa sana na kaka zake watatu na wazazi wake. Alikuwa mcheshi na mwenye maarifa ya kibiashara. Mungu amlaze mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment