Wednesday, October 10, 2012

LADY JAYDEE AJIPANGA KUTOKA NA KIPINDI CHA TV MWEZI HUU




Baada ya kufanya vizuri kwenye biashara zake hasa ile inayoendelea Nyumbani Lounge, mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee, amesema katikati ya mwezi huu ataanza kuonekana kwenye kipindi chake cha TV.

Hata hivyo mwanamuziki huyo hajasema jina la kipindi hicho na wapi kitakuwa kikionekana na amewataka mashabiki wake wabashiri.


“Habarini za Leo, Nimerudi tena. Kutoa jibu la Project yangu mpya… NI KIPINDI CHA TV, ila nahitaji washindi zadi, Unaweza kubahatisha ni Kituo gani cha TV kitakachorusha kipindi hicho na Kipindi kitaitwaje????? washindi 5 watashirikishwa katika hafla ya ufunguzi wa kipindi hicho October 2012… Kazi ni kwenu,”ameandika leo kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Amesema washindi watatu watakaopatia watapata CD ALBUM YA.5, Complimentary za kuingia MACHOZI BAND miezi 3 pamoja na kula lunch au dinner pamoja na yeye siku ya utambulisho wa project hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...