Thursday, May 3, 2012

WASTARA, SAJUKI NDOA YA MATESO





UKWELI ni kwamba mastaa wawili wakubwa wa filamu za Kibongo ambao ni wanandoa, Wastara Juma na Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ hawajawahi kufurahia maisha ya ndoa yao tangu walipooana Juni 6, 2009 kufuatia kuandamwa na mikosi kila kukicha...

Katika maisha yao ya ndoa, wawili hao wamekuwa wakipokezana mateso huku likiibuka jipya la kuwatoa machozi mara kwa mara na sasa Sajuki ndiye anayewaliza watu kufuatia kusumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni.

Ili kushibisha hoja kuwa wawili hao hawajawahi kuwa na furaha, shuka na data zifuatazo;

MACHI 12, 2009
Wakiwa wachumba, Wastara na Sajuki walipata ajali mbaya ya ‘bodaboda’ maeneo ya Tabata, Dar es Salaam ambapo mwanadada huyo alikatika mguu, hapo ndipo furaha ya wawili hao ilipoanza kutoweka.

MWAKA 2010
Baada ya kufunga ndoa, miezi kumi ya mwaka 2010, maisha hayakuwa mazuri kwani Wastara aliishi bila mguu mmoja hadi alipowekewa wa bandia Nairobi, Kenya ukiwa na gharama ya Sh. milioni 7.

AGOSTI 29, 2011
Wastara alikimbizwa hospitalini na kulazwa baada ya kubainika kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa nimonia.

Hata hivyo, baadaye ilibainika kuwa alikuwa mjamzito lakini alificha kwa kuwa aliogopa lolote linaweza kutokea kwani alikuwa akisemwa juu ya kutopata mtoto, hivyo kupoteza raha ya ndoa yao.

OKTOBA 29, 2011
Machozi mengine! Sajuki naye aliripotiwa kuwa hoi kitandani akisumbuliwa na uvimbe tumboni ambapo zilihitajika Sh. milioni 6 kwa ajili ya matibabu hivyo kupoteza kabisa furaha ya wanandoa hao.

MACHI 7, 2012
Wakati Sajuki bado mgonjwa akijiandaa kwenda kutibiwa nchini India, ndoa yao ilipata uzao wa kwanza, lakini hawakuweza kufurahia kwa sababu jamaa huyo yuko hoi.

APRILI 2, 2012
Sajuki alirejea kutoka katika Hospitali ya Apollo nchini India alikopeleka vipimo vya afya yake na kupata matibabu ambapo alisema alikuwa amepata nafuu kidogo kabla ya hivi karibuni hali kuwa mbaya zaidi na kuibua vilio upya ambapo kila Mtanzania anaombwa kutoa mchango wake wa hali na mali ili arudishwe India.

MCHANGO
Ili kumchangia Sajuki akatibiwe, tuma Tigo Pesa kwenda namba 0713 666 113 au akaunti ya Benki ya Akiba Commercial namba 050000003047 yenye jina la Wastara Juma Issa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...