Tuesday, May 15, 2012

WATOTO HAWA NI MAAJABU YA MUNGU


Mtoto aliyezaliwa mjini Songea akiwa na nyeti usoni.

Mtoto aliyezaliwa jijini Lagos akiwa ameshikilia Kurani mkononi.


WATOTO wawili walioripotiwa kuzaliwa, mmoja mjini Songea akiwa na nyeti usoni na mwingine akiwa ameshikilia Kurani mkononi huko Lagos, Nigeria wiki iliyopita, wametajwa kuwa ni maajabu ya Mungu.

Baadhi ya wananchi waliozungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, walitaja matukio hayo kama ni njia ya Mungu kuwakumbusha wanadamu kuwa yupo na si vinginevyo.

Maalim Hassan Yahya Hussein amesema wanadamu wanapaswa kujua kuwa Mungu ana maajabu yake na ana uwezo mkubwa, hivyo mambo kama hayo kwake hayamshangazi kwa kuwa ni utashi wake.
Jijini Lagos, Nigeria mama Kikelomo Ilori (32), alijifungua Jumatatu iliyopita mtoto aliyekuwa ameshikilia Kurani ndogo baada ya kubeba mimba kwa miezi 10 na kwamba licha ya mumewe kumshawishi kuitoa mimba hiyo, alikataa.

“Nilipokataa kutoa mimba, mume wangu alinitelekeza akidai kuwa ‘hilo ni tatizo lako,’ lakini nesi aliyenizalisha alishangazwa na tukio hilo, akasema Kurani itupwe lakini nilikataa, nikasema mama yangu lazima aione,” alisema Kikelomo.

Mchungaji wa kanisa analoabudia mwanamke huyo, Victoria Yetunde Dada alisema wakati wa ujauzito, Kikelomo alikuwa akifika kanisani mara kwa mara kuomba na akamshauri asiitoe mimba hiyo kwa kuwa kiumbe hicho kimeletwa na Mungu.

Mkurugenzi wa madaktari katika Hospitali ya Ikeja jijini Lagos, Dr. Bode Tawak amesema kisayansi tukio hilo haliwezekani kutokea.

“Unajiuliza maswali mengi. Kurani iliingiaje kwenye mfuko wa uzazi? Kuna mambo ambayo huwezi kuelezea lakini Nigeria mambo mengi ya ajabu hutokea na huwezi kuyafafanua kisayansi,” alisema Dk. Bode.

Wakati hayo yatitokea nchini Nigeria, mjini Songea, Tanzania, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Stumai Ausi amejifungua mtoto wa ajabu katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, ambapo maumbile yake ya sehemu za siri yapo kichwani na wananchi kusema huo ni mpango wa Mungu.

Muuguzi mkunga wa hospitali hiyo, Philomena Mwingira, alisema mtoto huyo sasa amehifadhiwa katika chumba maalum kwa kuwa hawawezi kumuacha nje kwani nyeti zake zipo sehemu isiyo ya kawaida na kwamba wanaendelea kumfariji mama huyo kukubaliana na hali hiyo.

Hata hivyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Mathayo Chanangula, alisema mtoto huyo alizaliwa Aprili 25, mwaka huu, akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa. Alifafanua kuwa sababu za kitaalamu zilizosababisha mtoto huyo kuzaliwa katika hali hiyo ni unywaji wa dawa zisizostahili kwa mama mjamzito kabla ya kutimiza miezi mitatu ya ujauzito.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...