Unaamini katika ndumba? Tukio la kustaajabisha limetokea nchini Kenya ambapo mke wa mtu, aliyekuwa anazini na mume wa mtu, walikutwa wamegandana.
Watu hao (majina hayajawekwa wazi), walikutwa na aibu hiyo ya karne Jumatano iliyopita wakati wakitenda dhambi hiyo kwenye kitanda chakavu.
Inanyetishwa kuwa watu hao, walijitia hawaujui msemo wa mume/mke wa mtu ni sumu, hivyo wakadakana juu kwa juu kwenda kupeana mahanjumati.
Walipogundua tamu imejaa shubiri, walikuwa wameshachelewa kwani tayari jamii ilishajua tatizo lililokuwa linawasibu chumbani, watu wakawa wameshakusanyika mlangoni huku wengine wakitaka kutoa msaada na waliosalia wakishabikia kimbeya.
Baada ya polisi kuona hivyo, walimsihi mume wa mwanamke huyo ambaye alitoa sharti la kupewa shilingi elfu 20 za Kenya (shilingi 378,000 za madafu), na baada ya kukatiwa ‘fuba’ hilo, waliachiana.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alikaririwa akisema: “Huyu jamaa amekutwa kwa nyumba ya mtu akihanyahanya bibi ya mwenzake, naona ni uchawi sasa polisi waliwakuta wakiwa wameshikana hivyohivyo.”
Yapo madai kwamba fumanizi hilo lilitokea kwenye nyumba ya mume wa mke huyo aliyenasa, hivyo mfumaniwa huyo ni jasiri aliyepitiliza.
Yapo madai kwamba fumanizi hilo lilitokea kwenye nyumba ya mume wa mke huyo aliyenasa, hivyo mfumaniwa huyo ni jasiri aliyepitiliza.
Baada ya kupokea fedha za faini ya fumanizi, mwanaume huyo aliinua mikono kwamba hamtaki tena mkewe.
HII HAPA NI FULL VIDEO YA TUKIO...
No comments:
Post a Comment