Thursday, May 31, 2012

BAADA YA MTAJI, SASA DOGO ASLAY ANAMJENGEA MAMA NYUMBA…… ISIKILIZE SINGLE YAKE MPYA PIA.



Aslay.
Dogo Asley November mwaka jana alimpa mama yake mtaji wa laki tano kwa ajili ya kufanya biashara, leo ametangaza good news nyingine kuhusu kuwasaidia wazazi wake ambao maisha yao yamebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya kupewa mitaji ambayo wameweza kuiendeleza vizuri mpaka sasa.
Alichokitangaza leo Dogo Aslay mwenye umri wa miaka 16 ambae muziki pekee ndio unaompa hela, ni kuhusu kuwasaidia wazazi wake kujenga nyumba kwenye kiwanja ambacho kilinunuliwa na mama yake mzazi Gongo la Mboto Dar es salaam miaka kadhaa iliyopita, ametoa zaidi ya laki saba Mwaka huu kuifikisha nyumba mpaka kwenye madirisha na anachotaka ni kumaliza kuijenga ndani ya muda mfupi sana ujao.
Hiki sio kitu cha kawaida, dogo Asley amekua mtoto wa kwanza Tanzania mimi kumsikia akiwa na umri mdogo kama huo lakini katoa kiwango kiwango kikubwa cha pesa kama hicho kumjengea mama yake nyumba.
Aslay amesema “maisha tuliyotokea sisi sio mazuri, nitaendelea na moyo wangu huu huu kwa sababu nikiwaacha wazazi wangu nahisi kama laana itanipata, nataka nikifikisha miaka 17 niwe nimemaliza kumsaidia mama kujenga nyumba, uwezo huo ninao”
Staa huyu ambae single iliyompa nafasi ya kuingia kwenye list ya wakali wa bongo fleva ni naenda kusema kwa mama,  ametoa zawadi nyingine nzuri ya single mpya inaitwa Umbea umbea ambayo pia inahusu ukweli wa maisha ya mama yake ya kunyanyaswa na umbea umbea wa mtaani, kampa shavu Chege.
Isikilize single yake mpya ya Umbea Umbea hapo chini………………….. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...