Tuesday, May 29, 2012

DAKTARI WA KANUMBA AFYATUKA: ASINGEKUFA KANUMBA ANGEKUFA LULU




Elizabeth Michael 'Lulu'.

Marehemu Steven Kanumba.
BAADA mwigizaji kinda Elizabeth Michael 'Lulu' aliyepandisha KIZIMBANI jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiwa mshukiwa namba moja wa kifo cha Steven Kanumba, kauli aliyofyatua aliyekuwa daktari wa mastaa hao aliyetajwa kwa jina moja la Kidume ina ukakasi.
SIMU YA LULU KWA KIDUME
Kwa mujibu wa Kidume, usiku wa Aprili 6 kuamkia 7, mwaka huu (alipofariki Kanumba), Lulu alimpigia simu na kumweleza kuwa siku hiyo angekunywa pombe hadi afe bila kujali kuwa alikuwa kwenye dozi, jambo ambalo lingemhatarishia maisha yake.
“Lakini nilimwambia asinywe kwa sababu alikuwa na dozi, si unajua alikuwa na matatizo ya tumbo?
“Aliniomba anywe hata kidogo, nilipomkatalia akaniambia potelea mbali, siku hiyo lazima atoke akanywe sana,” alisema dokta huyo.
ALIJULISHWA JUU YA UGOMVI
Kidume aliendelea kufyatuka kuwa hata Lulu alipofika nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza-Vatican, Dar, alimpigia simu na kumwambia juu ya ugomvi wake na mwandani wake huku akimtahadharisha kuwa alikuwa amefungiwa ndani.
TAFSIRI RAHISI
Katika sentensi nyingine, Kidume anathibitisha kuwa kama marehemu asingemfungia ndani Lulu, angeenda kunywa pombe hadi afe kama alivyokuwa amemwambia na Kanumba angekuwa anadunda mtaani hivi sasa.
LULU ALIKUWA ANAUMWA NINI?
Bila kutaja ugonjwa, Kidume alidai kuwa Lulu alikuwa na matatizo ya tumbo na alikuwa akiwatibu wote wawili kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...