Friday, May 18, 2012

WASTARA, SAJUKI MKASA MPYAA!





Wastara Juma.

               Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
WAKATI wakiwa nchini India kwa matibabu, huku nyuma nyumbani kwa mastaa wanandoa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na Wastara Juma kumeibuka mkasa mpyaa...

Kwa mujibu wa Wastara, wakiwa katika Hospitali ya Saifee iliyopo jijini Mumbai nchini humo, walipokea taarifa mbofumbofu kutoka nyumbani kwao Tabata Barakuda, Dar es Salaam kuwa kuna matapeli waliojifanya waganga walifika kwenye familia wakitaka kumtibu Sajuki ilihali wakijua ameshapelekwa India....

TATIZO
“Kuna tatizo limetokea huko nyumbani Tanzania, kuna matapeli wanaifuata familia, wanajifanya ni waganga, wanataka kumtibia Sajuki,” ilisomeka sehemu ya maelezo ya Wastara aliyoyatuma kwa Mtangazaji wa Clouds FM, Dina Marios.

Wastara alieleza kuwa watu hao walitaka wapewe Sh. milioni
3.5 ili wamuokoe Sajuki kwa sababu kalogwa na mtu aliyemdhulumu hivyo ugonjwa wake siyo wa kwenda kutibiwa India.

“Ukweli sisi hatujawahi kumdhulumu mtu. Waganga hao wapo wengi wanaisumbua familia tangu tulipoondoka. 

“Naomba waache hiyo tabia si nzuri kwani wanatukwaza sana,” alisema Wastara, kauli iliyowatoa machozi Watanzania kwa mara nyingine kwani hadi akafikia hatua hiyo ina maana hali hiyo imewaumiza.

MATIBABU
Tofauti na ilivyokuwa ikiripotiwa kuwa Sajuki alikwenda kutibiwa katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi, India, Wastara alisema wapo katika Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai, India na madaktari walikuwa wakiendelea na vipimo.

“Tulifika salama, wamerudia tena vipimo ili wajue waanzie wapi,” alisema Wastara.

KINACHOMTESA SAJUKI
Kinachomtesa mwigizaji Sajuki ambaye pia ni prodyuza wa filamu ni uvimbe pembeni ya ini kitaalam ni dalili za ugonjwa wa Hepatoma (kansa ya ini).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...