Tuesday, May 29, 2012

UMRI WA LULU WAENDELEA KUWA KITENDAWILI



Kikosi maalum cha makomandoo wa Magereza wenye silaha nzito, kofia za chuma na mavazi ya kuzuia risasi wakishuka kikomando kuliwahi basi alilopakizwa Lulu.

Ulinzi umeimarishwa wakati Lulu akisubiriwa kushuka.

Akishuka chini ya ulinzi mkali.

Askari waliokuwa kwenye gari wakiwa tayari kumlinda msanii huyo.

...Akiwa ndani ya mahakama.

...Akitafakari jambo.

Kila mahali kulikuwa na askari eneo la mahakama.

Baba yake Lulu (kushoto) akiwa na wakili Kennedy Fungamtama anayeliongoza jopo linalomtetea msanii huyo.
KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu za maigizo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambayo leo imefanyika katika Mahakama ya Biashara kufuatia malumbano makali ya kujadili umri wake.
Kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa maamuzi hayo kama ana umri wa miaka 17 kama unavyodai upande wa utetezi au ni miaka 18 kama unavyodai upande wa mashitaka.
Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Dk. Fauz Twalib alisema ameshindwa kutoa maamuzi hayo kufuatia mjadala huo kuwa mrefu hivyo ameahidi kutoa maamuzi hayo Juni 11 mwaka huu saa nne asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...