Wednesday, May 9, 2012

UWOYA ATINGA NA MBWA KWENYE ‘BETHIDEI’






ICON mwenye mvuto wa kipekee katika tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya aliwashangaza watu baada ya kutinga kwenye ‘bethidei’ ya mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la mama Rolaa akiwa na mbwa huku kivazi chake kikiwa utata mtupu.
Macho mawili ya paparazi wetu yalishuhudia kituko hicho, juzi, Jumapili, nyumbani kwa mama Rolaa, Mbezi Beach jijini Dar.

Paparazi wetu aliuona mshangao waliokuwanao wageni waalikwa pale Uwoya ambaye alitinga ndani ya jumba la kifahari la mama huyo saa 2:00 usiku akiwa amembatana na mbwa huyo aliyekuwa amemfunga mnyororo na kumshikiria muda wote.

“Duh! Hii kali kuna swaga nyingi ambazo tunaziona lakini hii ya Uwoya too much,” alisikika mmoja wa wageni waalikwa aliyekuwa akameaa karibu na paparazi wetu.

Baada ya kupata picha kadhaa za Uwoya akiwa na mbwa wake, mwandishi wetu alimuuliza kisa cha kutinga na mbwa, ambapo alisema mbali ya kuwa ni swaga lakini alikuwa amekuja kukomesha wanafiki wanaomfuatilia.

“Hii ni komesho kwa wanafiki wanaopenda kujikweza kupitia jina langu, mimi sisemi nao, wakileta za kuleta watasema na mbwa wangu, vilevile ni moja ya swaga zangu mpya, najua kuna watu wataiga,” alisema Uwoya.

Katika hatua nyingine Uwoya aliwashangaza watu kwa jinsi alivyovaa nguo iliyokuwa na mpasuo wa nguvu ambao uliacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi.

“Jamani amesahau kama yeye ni mke wa mtu, hata kama mumewe hayupo? Kivazi kile mbona kinamuacha mtupu?” alihoji mtu mwingine aliyekuwa katika sherehe hiyo na kuwafanya wengine waangue vicheko.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...