Saturday, May 19, 2012

PICHA 17 ZA NYUMBANI KWA KINA KANUMBA SHINYANGA!


Hii ndio nyumba anayomiliki baba yake Kanumba huko Ngokolo Shinyanga, sehemu ya nyumba amepangishia watu wengine
Mimi nikifanya mahojiano na baba Kanumba ambae nilimfungia safari mpaka Shinyanga.
.
Hii picha ni ya cover la movie waliyocheza pamoja, Kanumba Johari na Ray, ni zawadi ambayo Marehemu Steven Kanumba alimzawadiwa baba yake, na imewekwa juu ya mlango wa kuingilia sebleni.
.
Huyu ni mdogo mwingine na Kanumba kwa upande wa baba ambae ameahidi kuingia kwenye soko la movie miaka miwili ijayo kwa sababu anaamini uwezo wa kuigiza anao.
Huyu pia ni mdogo mwingine wa Marehemu Kanumba ambae amethibitisha kwamba ana uwezo wa kuigiza, na mwaka jana alizungumza na kaka yake na alikua mbioni kumleta Dar es salaam ili kuigiza wote.
Huyu ndio mama wa hao wadogo zake Kanumba hapo juu.
.
Nyumba anayoishi Baba Kanumba na familia yake, pamoja na wapangaji.
Familia.
Kutoka kushoto ni kaka wa Marehemu Kanumba pamoja na wadogo zake kwa upande wa baba ambao wote wamekiri uwezo wa kuigiza wanao na wataingia kwenye filamu kuliendeleza jina la ukoo.
Hii ni shule aliyosoma Marehemu Kanumba, Ngokolo ni karibu na nyumbani kwa baba yake.
Wakati napita nilionyeshwa hapa kwamba ndio Nyumbani kwa kina Mwigizaji JOHARI, kumbe wanatoka sehemu moja na Kanumba, nilikua sijui.
Hili ndio kanisa la Ngokolo aliloanza kuigiza Kanumba akiwa na umri wa miaka mitano tu na alikua akiimba kwaya pia.
Hii ndio simu Kanumba aliyomnunulia baba yake mzazi mara ya mwisho kuonana june 2011, aliinunua kwa elfu 60 baada ya kukuta simu ya baba yake ni mbovu.
Hii ni nyumba ya baba Kanumba kwa nje, amepangisha watu kwenye hicho chumba cha duka pamoja na hicho kinyozi hapo kushoto.
Hii ndio Ofisi ya Marehemu Kanumba iliyopo Sinza Dar es salaam, sasa hivi inaendelea na kazi.
.
.
.
Huyo hapo kushoto ndio Zakayo Magulu, aliefanya kazi na Kanumba kwa miaka saba akiwa kama Director msaidizi, camerman na Editor.
Hii picha Kanumba ndio aliiweka ukutani kwenye duka lake.
Pembeni ya hilo duka kuna chumba cha kueditia, na pembeni Kanumba aliweka baadhi ya tuzo zake kati ya tuzo 28 alizowahi kushinda.
.
R.I.P STEVEN KANUMBA.
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza Makala yake ya dakika 16 kuhusu mazingira ya kifo chake na mambo mengine, isikilize hapo chini……

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...