Friday, November 2, 2012

VURUGU KATI YA WAUMINI WA DINI YA KISLAMU NA POLISI ZATOKEA TENA JIJINI DAR

VURUGU kati ya watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kiislamu na Polisi zimezuka tena leo katika eneo la Msikiti wa Idrisa uliopo Kariakoo jijini Dar es Salaam. Vurugu hizo zimeambatana na kutupwa kwa mabomu ya machozi kutoka kwa polisi waliokuwa wanajaribu kuzuia ghasia hizo. Baadhi ya waumini hao wametiwa nguvuni na jeshi la polisi. Awali usalama ulikuwa umeimarishwa katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kutokana na taarifa zilizokuwepo kuhusu maandamano ya waumini hao wa dini ya Kiislamu. 
Mwandishi wetu ameshuhudia askari wakiwa wametanda eneo la Ikulu Magogoni jijini Dar kuimarisha zaidi ulinzi. Nae Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa vijana wake wamejipanga vizuri kila kona kuhakikisha hakuna tukio lolote linalotokea ambalo litahatarisha amani ya nchi pamoja na wananchi wake.











No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...