Thursday, November 1, 2012

ROSE CHITALA AFANYA PATI YA POMBE KALI


MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Rose Chitala amewashtua mashosti wake baada ya kufanya sherehe yake ya kuzaliwa ‘bethidei iliyotawaliwa na pombe kali.

Moshosti wa Rose waliohudhuria pati hiyo.
Ishu hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ‘prizenta’ huyo aliwaalika marafiki mbalimbali ambao wengine walishindwa kushiriki vinywaji hivyo kwa  sababu hakukuwa na bia na kubaki wakishangaa.

“Jamani vinywaji ndiyo kama hivi mnavyoviona, nyama choma zipo za kutosha hivyo msiogope tumieni viishe,” alisema Rose akielekeza mkono kwenye meza iliyokuwa imesheheni pombe kali tupu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...