Thursday, November 1, 2012

SUMALEE AIBIWA GARI


MSANII wa kitambo kunako gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo, Ismail Sadick ‘Suma Lee’, ameibiwa gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T504 BRF, Erick Evarist anashuka nayo.

Ismail Sadick ‘Suma Lee’.
Akichonga na Amani, Suma aliweka wazi kuwa kisanga hicho kilimtokea Jumapili iliyopita mishale ya saa kumi na mbili za jioni katika Ufukwe wa Coco alikoenda kula bata na washkaji zake.

“Baada ya kuibiwa gari, nilienda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kuandikisha jalada lenye namba OB/RB/19237/2012 WIZI WA GARI.  Kiukweli wamenirudisha nyuma sana kimaendeleo, namuomba Mungu lipatikane vinginevyo nitakuwa nimelostika kinoma,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...