Thursday, November 1, 2012

MAMA RAY C: SITAKI KUMWONA LORD EYEZ NYUMBANI KWANGU


MAMA mzazi wa staa wa Bongo Fleva mwenye skendo ya kubwia madawa ya kulevya, Rehema Chalamila  ‘Ray C’, Magret Mtweve ametoa tamko kali dhidi ya aliyekuwa mpenzi wa mwanae, Isaac Makuto ‘Lord Eyez’ kutotia mguu nyumbani kwake Kunduchi, Dar.

Mama mzazi wa Rehema Chalamila  ‘Ray C’, Magret Mtweve.
Mama Ray C alichimba mkwara huo wakati akizungumza na HOT POT Jumatatu iliyopita alipoulizwa kama Ray C amerudi nyumbani kwake baada ya kutoweka kitambo.
“Amerudi jana jioni (Jumapili). Nilipomuuliza amesema alikuwa Kariakoo, lakini hataki kuwataja aliokuwa nao wala alichokuwa akikifanya.
Isaac Makuto ‘Lord Eyez’.
“Nimekuwa nikizunguka kwenye makanisa mbalimbali kumuombea njia, naona ameanza kuleta matumaini lakini sitaki kabisa kumsikia mtu anayeitwa Lord Eyez, yeye na wenzake ndiyo waliomsababishia matatizo haya mwanangu,” alisema mama huyo.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...