Thursday, November 1, 2012

GARI LA MILIONI 70 LA MSANII SUMALEE LAIBWA.


Sumalee amedai kwamba hili gari lake liliibiwa maeneo ya Coco beach baada ya kulipaki na kwenda kukutana na mtu, muda mfupi baadae aliporudi akalikosa ambapo mtu aliekua jirani alimwambia kwamba kuna watu wamelichukua kama lao, hawakuvunja kioo wala kuharibu chochote yani walilifungua kama lao na mziki wakawasha kabla ya kuondoka, tayari amesharipoti polisi.
Gari hili ambalo halijafikisha hata mwaka toka Suma Lee alinunue thamani yake ni milioni 70, gari lake aina ya Rav 4 pia aliloliuza kabla liliwahi kutaka kuibiwa Kariakoo mwanzoni mwa mwaka huu ambapo watu walilifata kabisa mpaka linapolazwa ila waliokua karibu ndio wakashtukia mchezo.
Kwenye Exclusive interview  Sumalee amesema gari hili ambalo alipata nalo ajali Kigoma mwaka huu akiwa na wasanii wenzake akiwemo Linex, huwa haliazimi ovyo hivyo hakuna uwezekano kwamba wizi huo umefanya na mmoja kati ya marafiki zake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...