Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.
Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo. ..
Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.
Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
Baada ya kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.
Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.
Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo.
habari zaidi endelea kuchungulia hapahapa .
Mwili wa Sharo utazikwa kesho jioni.
No comments:
Post a Comment