Thursday, November 8, 2012

MAMA KANUMBA, SETH VILIO VINAENDELEA...


MIEZI saba tangu msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba kuiaga dunia Aprili 7, 2012 bado majonzi na vilio vimeendelea kuitikisa familia yake ambapo hivi karibuni mama yake, Flora Mtegoa na mdogo wake, Seth Bosco waliangua vilio upya juu ya kaburi lake.
Mama Mzazi wa Steven Kanumba, Flora Mtegoa akilia juu ya kaburi la mwanae.
Tukio hilo lilishuhudiwa na paparazi wetu Novemba 4, mwaka huu ambapo mama Kanumba na Seth walifika katika kaburi alilozikwa Kanumba, Kinondoni, Dar huku wamebeba maua ikiwa ni mara ya kwanza kulitembelea rasmi kaburi hilo tangu lifanyiwe ukarabati upya.
Mdogo wake Marehemu Kanumba, Seth Bosco akiweka shada la maua katika kaburi la kaka yake.
“Mimi sitaacha kumlilia mwanangu Kanumba jamani na siwezi kumsahau maana kifo chake kilikuwa cha ghafla sana wakati tulikuwa tumepanga mambo mengi. 
“Nina muda sijaja kuliona kaburi lake, tangu lilivyojengwa upya sijafika ndiyo leo nakuja huku kwa ajili ya kuliona na kulifanyia usafi. Maskini mwanangu, lala kwa amani baba,” alisema mama huyo huku akilia kwa uchungu ambapo Seth naye alishindwa kujizuia.

Mama Kanumba na Seth wakisali katika kaburi la Kanumba.
Mama Kanumba na Seth wakilifanyia usafi kaburi la Kanumba.
Mama Kanumba akilia mbele ya kaburi la mwanae.
Kaburi la Mwigizaji mahiri, marehemu Steven Charles Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Ujumbe ulio kaburini hapo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...