Monday, November 5, 2012

HIKI NDICHO ALICHOSEMA RUGE MUTAHABA KUHUSU ISHU YA RAY C NA UTUMIAJI DAWA ZA KULEVYA....


Taarifa zilizoenea town sasa hivi kuhusu mwimbaji Ray C ni kwamba anadaiwa kuwa mteja sana wa dawa za kulevya kutokana na kuzidisha matumizi.
Baada ya hili gazeti kutoka wiki iliyopita watu wengi wamezungumza na Mr Ruge Mutahaba ambae ni mdau mkubwa wa muziki wa Tanzania ambae pia amewahi kuwa meneja wa Ray C wakiuliza kwa nini hakijafanyika kitu chochote kumsaidia Ray C.
Namkariri Ruge akisema “sio kwamba ameachwa, mtu anapopata matatizo hatua ya kwanza ya kuyatibu matatizo hayo ni yeye mwenyewe kuyakubali, uzuri ni kwamba yeye mwenyewe amekubali kuna matatizo amekuja sehemu anayohitaji kusaidiwa, mipango ya kusaidiwa imeanza siku nyingi… ipo na inaendelea kwa hiyo zinapotoka picha kama hizi wakati mwingine inaweza ikawa inavunja moyo hata kwa yule anaepigana na mazingira kama yale”
“Alishaanza hatua ya kwanza ya matibabu, anafanya bidii kwenda kwenye hatua ya pili ya matibabu, kweli kabisa anafanya bidii na kuhusu taarifa kwamba amepelekwa Iringa kupata matibabu ya kuacha utumiaji wa dawa za kulevya hakuna ukweli wowote, kuna taarifa nyingi za kupotosha ambazo mimi nilikua naomba watu wangeacha kuzisambaza kwa sababu hazisaidii mtu yeyote yule na vilevile zinaendelea kulikuza tatizo” – Ruge

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...