Thursday, November 1, 2012

MAMA AJA JUU MWANAYE KUTESWA KWENYE FILAMU


MAMA wa mlemavu wa kwenye filamu ya Mwaka wa Shetani, Bongebonge (pichani) amemjia juu nyota wa filamu hiyo, Chetu Omar ‘Ney’  aliyecheza kama mama wa kambo wa kijana huyo na kumtesa.

Mama wa mlemavu huyo baada ya kuona filamu hiyo ambayo mwanaye ameshiriki kuteswa, alimvutia ‘waya’ Ney na kumjia juu  akimuuliza kama yeye amewahi kuzaa kwani aliumizwa na ukatili wake katika filamu hiyo.

Akizungumza na safu hii, Ney alisema yeye ni mama mwema ila kwenye muvi hiyo aliuvaa uhusika ndiyo maana mama wa Bongebonge alimjia juu.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...