Thursday, November 1, 2012

JAMILA: JAMANI MIMI SIYO ‘HAUSIGELI’ WA WEMA SEPETU


MWANADAFADA aliyezaa na msanii wa Bongo Fleva, Amani Temba kutoka TMK Wanaume, Jamila Msafiri amefunguka kuwa anakerwa sana na tabia ya baadhi ya watu kumpakazia kuwa yeye ni hausigeli wa Wema Sepetu kutokana na ukaribu walionao wawili hao, Imelda Mtema anashuka nayo.

Wema Sepetu.
Akichonga na Amani, Jamila alisema Wema ni rafiki yake kama walivyo marafiki wengine na kutaka watu waache kutafsiri tofauti kwani wanamkosesha raha.

“ Kwa nini mtu anapokuwa karibu na Wema wanampachika majina ya ajabu ajabu? Hata Snura naye walimpachika majina ya ajabu, kwani Wema hawezi kuwa na rafiki? Hata Obama ana marafiki sembuse Wema,” alisema Jamila.


Jamila Msafiri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...