Thursday, November 1, 2012

BUNGENI PAMENUKA UPYA


UPEPO mbaya uliotokana na skendo ya rushwa bungeni wakati wa Bunge la Bajeti ya mwaka 2012-2013, umenuka upya, huku chini kwa chini kukiwa na shinikizo kutoka kwa wabunge wanaotaka ripoti ya kamati ya Brigedia Mstaafu, Hassan Ngwilizi isomwe bungeni.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Sarah Msafiri ambaye ni mmoja wa waliotuhumiwa.
Wakati kukiwa na shinikizo hilo la kumtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuruhusu ripoti ya Ngwilizi isomwe bungeni, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Sarah Msafiri ambaye ni mmoja wa waliotuhumiwa, ameamua kufunguka.
Sarah amesema baadhi ya watu wamekuwa wakifanya kampeni za kumchafua kwa makusudi.

Alisema: “Nimeshtushwa sana na taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari kunihusisha mimi na Kampuni ya M/S Sharrifs Services & General Supply iliyokuwa ikifanya biashara na Tanesco na kudai kwamba nilisimamia malipo yenye utata kutoka Shirika la Tanesco.”

Akaongeza: “Tuhuma hizo ni uzushi mtupu. Mimi siyo mmiliki wa kampuni hiyo, sina hisa yoyote wala sijaajiriwa na kampuni hiyo.”
Sarah pia alitoa onyo kwa vyombo vya habari vilivyoandika habari alizoziita  za “mkakati wa kumchafua”, vimuombe radhi, vinginevyo atavichukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, naye alimueleza mwandishi wetu kwamba Spika Makinda hatafanya kitu kinachoeleweka kama hataruhusu ripoti isomwe bungeni.

Alisema, anatambua kuna namna ambayo inafanywa kulinda madudu ambayo yamegundulika kwenye ripoti ya Ngwilizi, hivyo unasukwa mpango ili isomwe kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge badala ya bunge zima.



Zitto pia ni mmoja wa waliotuhumiwa ‘kuvuta’ ndiyo maana yeye na wenzake, akiwemo Sarah, wanaoamini walisingiziwa, wamekuwa wakishinikiza ripoti isomwe waziwazi ili iwasafishe katika skendo hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...