Friday, November 30, 2012
VIDEO YA GARI ALILOPATA NALO AJALI SHARO MILIONEA
PICHA 13 ZA ENEO ALILOPATA AJALI SHARO MILIONEA, TAZAMA AJALI ILIPOANZIA.
Kingine alichoniambia huyu shuhuda ni kwamba kwenye hilo eneo huwa hakutokei ajali za mara kwa mara, kwa miaka zaidi ya 20 aliyoishi hapa ni ajali chache sana zimetokea, hakuna ajali mwaka huu zaidi ya Sharo Milionea ila mwaka jana ilitokea ajali moja ambapo mtoto wa shule aligongwa na basi la Raha Leo na kufariki.
Hili eneo liko umbali wa kama dakika 40 mpaka Tanga mjini na ni dakika 15 tu mpaka kufika nyumbani kwa kina Sharo milionea ambako ndiko Marehemu alikua anaelekea, rafiki yake wa karibu mwigizaji Kitale (anaeigiza kama teja) kasema mara ya mwisho Sharo aliongea nae na akamwambia anakimbia Tanga mara moja kumpelekea mama yake mtaji wa shilingi milioni sita za biashara ambazo alikua nazo wakati huo kwenye gari lakini imefahamika kwamba hizo pesa zimeibwa zote kwenye eneo la ajali.
HII NI VIDEO YA ENEO ALILOPATA AJALI SHARO MILIONEA NA JINSI ILIVYOKUA.
PICHA ZAIDI ZA SIKU YA MSIBA WA SHARO MILIONEA
Subscribe to:
Posts (Atom)