Saturday, August 4, 2012

UTAJIRI WA WA BAADHI YA WABUNGE UNATISHA



SAKATA la wabunge saba kuhusishwa kuomba na kupokea ‘kitu kidogo’ lililotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu limeingia katika sura mpya baada ya wananchi kuhamaki kwa habari zilizoripotiwa wiki hii kuwa kuna wabunge wana utajiri wa kupitiliza...
Baadhi ya wapiga kura wamesema kuwa kama ni kweli kuwa waheshimiwa hao wana utajiri mkubwa kiasi hicho, itabidi kuwafikiria upya mwaka 2015 kwa kuwa hakuna sababu ya kumpa kura mtu ili akale huku wapiga kura wakishinda na njaa.
Yapo madai mazito kwamba baadhi ya wabunge hao wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda wanamiliki maghorofa, magari ya kifahari wanayokodisha, vituo vya mafuta huku wengine wakidaiwa kuwa wazabuni wa mafuta migodini na wamiliki wa makampuni ya utalii (tours).
Wabunge wa CCM waliotajwa na Lissu kuhusishwa na kashfa hiyo na majimbo yao kwenye mabano ni Nassir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.
Wabunge wengine watatu waliotajwa na Lissu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.







No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...