Thursday, August 9, 2012

BAADA YA KUFUNGA DUKA LA NGUO, HII NDIO BIASHARA ANAYOIFANYA SASA MSANII CHEGE WA TMK FAMILY.


.
Chege amesema sehemu hii aliyofungua barber shop ndio ile ile aliyokua akiitumia kuuza nguo kwenye duka lake alilokaa nalo kwa mwaka mmoja na biashara kwenda vizuri bila kumpa hasara ambapo kwa siku alikua anaingiza kuanzia shilingi laki mbili mpaka laki nne.
Kilichomfanya abadili biashara ni ushauri alioupata kuhusu urahisi wa biashara ya barber shop kwa sasa ambayo pesa zake zinatembea haraka kuliko duka la nguo.
Kwenye nyumba alipoiweka hii biashara yake mpya analipa kodi ya shilingi laki mbili kwa mwezi ambapo ametumia shilingi milioni nane kwenye kufanya marekebisho ya kutoka kwenye duka la nguo mpaka barbershop ambayo imetoa ajira kwa vijana watano.
Kuhusu kuweka hizo picha za wasanii wenzake wa TMK kwenye vioo vya barbershop Chege amesema amefanya hivyo kwa sababu hiyo ni familia yake, anaipenda TMK wanaume family.. ambapo hizo picha mbili juu kabisa za 50 CENT na TEMBA amesema ni marepper ambao anawakubali sana.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...