Aug 1 2012 Jumatano jioni kilichoandikwa kwenye website ya club ya soka ya Azam Fc kuhusu mchezaji wao Mrisho Ngasa kuuzwa ghafla ni hiki, “Biashara na Mjadala wa Mrisho Ngasa umefungwa leo mchana saa tisa kasorobo baada ya Simba SC kuizidi nguvu Yanga na kutoa shilingi milioni 25, ofa ya Yanga iliiishia milioni 20″
Azam FC inamtakia kila la heri na mafanikio mema Mrisho Ngasa kwenye klabu yake mpya ya Simba.
Hayo yote ni maelezo yaliyotolewa kwenye website ya Azam Fc ambapo mpango wa kumuuza haukuwepo kabisa, umekuja ghafla baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kagame Cup.
kama bado unashangaa kwa nini Ngasa ameuzwa mapema hivi nataka kukwambia kwamba juzi yani Jumanne july 31 kwenye website ya Azam kuliandikwa hivi “Hadi hivi sasa Ofa ya Simba ni shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20, kutokana na hilo Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya Mwisho. Ingawa tungependa kumuuza Mrisho Ngasa Yanga lakini tutampeleka kwa timu iliyotoa ofa nzuri zaidi”
Kwenye sentensi nyingine wakaandika “Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu ambayo atacheza kwa raha na amani kutokana na yeye kuivaa na kuibusu Jezi ya Yanga siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga… Azam FC inaamini kuwa Yanga ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho, lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa na haja na Mrisho na ndiyo maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana, Kutokana na sababu hizo Azam FC italazimika kumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani hatuhitaji kuwa na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand ya Azam FC ambayo tunajaribu kuijenga” – Azam Fc
Imefahamika kwamba kitendo cha Ngasa kuivaa na kuibusu jezi ya Yanga ndio kitu pekee kilichowakasirisha maboss wa club hiyo na kuamua kumuuza mchezaji huyo ambapo Azam walitoa taarifa za kumuuza mchezaji huyo July 30 2012 na kuandika kwamba “Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu yoyote kumnunu mchezaji Mrisho Ngassa kwa gharama ya $ 50,0000″
“Azam FC imefikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo na badala yake kuipenda klabu aliyotoka ya Yanga hivyo uongozi wa klabu unapokea maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji, Ngassa anauzwa siku chache baada ya kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu logo ya timu hiyo, baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika mashindano ya Kombe la Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu” – Azam F
c
c
No comments:
Post a Comment