Thursday, August 9, 2012

EXCLUSIVE: HILI NDIO GARI JIPYA ALILONUNUA MSANII OMMY DIMPOZ.


Toyota RAV 4 ambayo thamani yake ni milioni 27 ndio kainunua staa wa hit single ya NAI NAI pamoja na BAADAE, ni mkali wa bongo fleva OMMY DIMPOZ.
Mshindi huyu wa tuzo mbili za KTMA 2012 amesema ni gari lake la kwanza kununua na ni kutokana na pesa ya muziki peke yake ambapo toka ameanza kuwa solo artist,  show yake ya kwanza kuifanya ilikua november 2011.
Ommy Dimpoz amesema pesa zote za kulinunua hili gari imetokana na pesa alizolipwa kutoka kwenye show alizofanya, kwa sasa pia yuko kwenye harakati za kukamilisha ujenzi wa nyumba yake Tegeta Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...