WAKATI utafiti ukiendelea kufanyika duniani kuhusu masuala ya afya, suala la ubora wa maziwa kiafa nalo limeangaliwa kwa makini. Ni ukwel ulio wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakiambiwa kuwa maziwa ni miongoni mwa vinywaji bora kwa binadamu na kwamba ndiyo chimbuko pekee la madini aina ya ‘kashiamu’. Hata hivyo, siyo tu maziwa huwaletea madhara baadhi ya watu, bali imegundulika ni chanzo cha magonjwa.
MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO
Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko kitu kingine. Vile vile siyo tu maziwa ya mama ni bora kwa mtoto, bali pia vilivyomo ndani ya maziwa hayo ni vya kipekee na haviwezi kupatikana katika vyakula vingine. Kwa maana hiyo maziwa ya mama ni maalum kwa mtoto tu.
Viumbe vinatofautiana namna vilivyoumbwa. Kwa mfano, Ng’ombe anapozaliwa hadi kukua huchukua muda wa mwaka mmoja kukomaa kimwili. Binadamu huchukua muda wa miaka 16 au zaidi kufikisha umri wa kukomaa kimwili, ikiwa ni pamoja na kubalehe kwa mtoto wa kike au kiume. Hii ina maana kwamba virutubisho vilivyomo kati ya jamii ya viumbe fulani ni tofauti na jamii nyingine.
Mtoto anapoanza kukua, mazingira ya tumbo nayo hubadilika ambapo huanza kulishwa vyakula vigumu kiasi na idadi ya vyakula anavyolishwa huongezeka. Hata hivyo, wengi wa watoto wanapoanza kupewa maziwa ya kopo huanza kuharisha, wengine hufunga choo kwa siku kadhaa na wengine hushindwa kuyanywa kuonyesha kutokubalika mwilini.
CHANZO BORA CHA ‘CALCIUM’
Mboga za majani ya kijani ni miongoni mwa mboga zenye kiwango kikubwa cha virutubisho vingi, vikiwemo ‘amino acids’, ‘omega 3’ na nyingine nyingi. Aidha, mboga za majani zinaelezwa pia kuwa chanzo kizuri cha madini ya ‘calcium’ na ‘magnesium’ ambayo husaidia ukuaji wa mifupa mwilini. Hivyo siyo lazima kunywa maziwa tu ili kupata madini hayo.
TAHADHARI MAZIWA YA PAKETI
Kwa mujibu wa watafiti wengi, maziwa ya paketi, ambayo kitalaamu hujulikana kama ‘Pasteurized Milk’ au ‘Homogenized Milk’, huwa ndiyo chanzo cha magojwa mengi. Kwa kawaida maziwa ya paketi hupitia hatua ya uchemshwaji kiwandani ili kuua vijidudu vinavyosababisha kifua kikuu (tuberculosis).
Pamoja na kupitia hatua hiyo kwa lengo la kuua vijidudu, lakini virutubisho muhimu vilivyomo kwenye maziwa navyo hupotea kutokana na joto kali linalotumika kuchemshia. Katika kujua madhara ya maziwa ya paketi, utafiti ulifanywa ukihusisha watoto 70 ambao walipewa maziwa mabichi kwa muda wa miaka mitano ni mmoja tu kati yao ndiye aliugua, lakini idadi hiyo hiyo waliopewa maziwa ya paketi, 14 waliugua!
Dk. Kurt Osler ni daktari bingwa wa moyo (Cardiologist) kutoka Jimbo la Connectcut nchini Marekani na amekuwa akifanya utafiti kuhusu maziwa ya paketi kwa muda wa zaidi ya miaka 20. Utafiti wake umeonesha kuwa maziwa ya paketi (homogenized milk) husababisha kolestro mbaya mwilini.
Dk. William Ellis ni mtaalamu wa mifupa, naye katika utafiti wake ameona kuwa maziwa yanahusika kwa kiasi kikubwa na magonjwa mbalimbali kwa watoto na watu wazima, kama vile uchovu, upungufu wa damu, maumivu ya tumbo, kuharisha, magonjwa ya moyo na mzio (allergies).
Watafiti kuhusu ubora wa maziwa wameeleza kuwa kama kweli maziwa ya ng’ombe yangekuwa ndiyo chanzo bora cha madini ya ‘calcium’, basi ugonjwa wa mifupa usingekuwepo kwenye maeneo ambayo watu hunywa maziwa kwa wingi, badala yake hali imekuwa kinyume.
Kwa ujumla, kama ilivyo hata kwa vyakula vingine, maziwa ni miongoni mwa vinywaji vinavyotakiwa kutumiwa kwa uangalifu na kwa usahihi, kinyume na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwetu kuwa maziwa hayana madhara yoyote kwa binadamu.
No comments:
Post a Comment