Wednesday, August 29, 2012

JE TID ALIPANGA KUMUUA ALI KIBA?!?


Anga la muziki wa Tanzania limekumbwa na jinamizi jipya , ambapo mwanamuziki mmoja anadaiwa kupanga kumuua mwanamuziki mwingine.....kama ni kweli itakuwa ni hatua mpya kabisa katika anga za muziki kwa miaka mingi. Mara ya mwisho tasnia ya muziki kukumbwa na mambo ya mwanamuziki kuuwawa ni miaka ya sabini wakati mwanamuziki mmoja wa Orchestra Makassy alipokutwa kachinjwa katika bafu. Mungu apishe mbali. Haya ndio yanayozungumzwa katika mitandao mbalimbali leo hii....
Inasemekana meneja wa Ali Kiba amesema yafuatayo......

"Baada sasa ya taarifa hizo  kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale anapoishi Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kupeleleza eneo lile.
 Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata. 

Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hilo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndio anahusika. 
Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."
  
Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba....TID mwenyewe alikuwa na haya yakusema......
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”

Tuesday, August 28, 2012

BABU LOLIONDO NI TAPELI




SERIKALI imethibitisha kuwa kitendo alichokuwa akifanya babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile, cha kutoa dawa ya kutibu magonjwa, ukiwemo Ukimwi aliyokuwa amedai kuwa ameoteshwa na Mungu ni cha kitapeli.

 Utafiti umebaini kwamba dawa hiyo  ya babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.

Kwa mujibu wa  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa Ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa, umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.
Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.
“Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.
Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini,  Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.
Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko.
 Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.
“Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama  vya Watu  Wanaoishi  na Virusi vya Ukimwi  nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya,  ameitupia  serikali   lawama  kwa  kuipigia  debe dawa  ya Babu  na  kuwafanya  wagonjwa  kutoroka hospitali huku wengi  wao wakiacha  kuendelea na  dawa wakiamini  wangepona  baada ya kunywa kikombe kimoja .
“Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe  mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma  toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa  kumfungulia  kesi.
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba,  amesema babu huyo siyo  mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi.
Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando   wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha  mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia  fedha kwa njia ya udanganyifu.

UKWELI KUHUSU MAZIWA YA NG’OMBE



WAKATI utafiti ukiendelea kufanyika duniani kuhusu masuala ya afya, suala la ubora wa maziwa kiafa nalo limeangaliwa kwa makini. Ni ukwel ulio wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakiambiwa kuwa maziwa ni miongoni mwa vinywaji bora kwa binadamu na kwamba ndiyo chimbuko pekee la madini aina ya ‘kashiamu’. Hata hivyo, siyo tu maziwa huwaletea madhara baadhi ya watu, bali imegundulika ni chanzo cha magonjwa.

MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO
Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko kitu kingine. Vile vile siyo tu maziwa ya mama ni bora kwa mtoto, bali pia vilivyomo ndani ya maziwa hayo ni vya kipekee na haviwezi kupatikana katika vyakula vingine. Kwa maana hiyo maziwa ya mama ni maalum kwa mtoto tu.
Viumbe vinatofautiana namna vilivyoumbwa. Kwa mfano, Ng’ombe anapozaliwa hadi kukua huchukua muda wa mwaka mmoja  kukomaa kimwili. Binadamu huchukua muda wa miaka 16 au zaidi kufikisha umri wa kukomaa kimwili, ikiwa ni pamoja na kubalehe kwa mtoto wa kike au kiume. Hii ina maana kwamba virutubisho vilivyomo kati ya jamii ya viumbe fulani ni tofauti na jamii nyingine.
Mtoto anapoanza kukua, mazingira ya tumbo nayo hubadilika ambapo huanza kulishwa vyakula vigumu kiasi na idadi ya vyakula anavyolishwa huongezeka. Hata hivyo, wengi wa watoto wanapoanza kupewa maziwa ya kopo huanza kuharisha, wengine hufunga choo kwa siku kadhaa  na wengine hushindwa kuyanywa kuonyesha kutokubalika mwilini.
CHANZO BORA CHA ‘CALCIUM’
Mboga za majani ya kijani ni miongoni mwa mboga zenye kiwango kikubwa cha virutubisho vingi, vikiwemo ‘amino acids’, ‘omega 3’ na nyingine nyingi. Aidha, mboga za majani zinaelezwa pia kuwa chanzo kizuri cha madini ya ‘calcium’ na ‘magnesium’ ambayo husaidia ukuaji wa mifupa mwilini. Hivyo siyo lazima kunywa maziwa tu ili kupata madini hayo.

TAHADHARI MAZIWA YA PAKETI
Kwa mujibu wa watafiti wengi, maziwa ya paketi, ambayo kitalaamu hujulikana kama ‘Pasteurized Milk’ au ‘Homogenized Milk’, huwa ndiyo chanzo cha magojwa mengi. Kwa kawaida maziwa ya paketi hupitia hatua ya uchemshwaji kiwandani ili kuua vijidudu vinavyosababisha kifua kikuu (tuberculosis).
Pamoja na kupitia hatua hiyo kwa lengo la kuua vijidudu, lakini virutubisho muhimu vilivyomo kwenye maziwa navyo hupotea kutokana na joto kali linalotumika kuchemshia. Katika kujua madhara ya maziwa ya paketi, utafiti ulifanywa ukihusisha watoto 70 ambao walipewa maziwa mabichi kwa muda wa miaka mitano ni mmoja tu kati yao ndiye aliugua, lakini idadi hiyo hiyo waliopewa maziwa ya paketi, 14 waliugua!
Dk. Kurt Osler ni daktari bingwa wa moyo (Cardiologist) kutoka Jimbo la Connectcut nchini Marekani na amekuwa akifanya utafiti kuhusu maziwa ya paketi kwa muda wa zaidi ya miaka 20. Utafiti wake umeonesha kuwa maziwa ya paketi (homogenized milk) husababisha kolestro mbaya mwilini.
Dk. William Ellis ni mtaalamu wa mifupa, naye katika utafiti wake ameona kuwa maziwa yanahusika kwa kiasi kikubwa na magonjwa mbalimbali kwa watoto na watu wazima, kama vile uchovu, upungufu wa damu, maumivu ya tumbo, kuharisha, magonjwa ya moyo na mzio (allergies).
Watafiti kuhusu ubora wa maziwa wameeleza kuwa kama kweli maziwa ya ng’ombe yangekuwa ndiyo chanzo bora cha madini ya ‘calcium’, basi ugonjwa wa mifupa usingekuwepo kwenye maeneo ambayo watu hunywa maziwa kwa wingi, badala yake hali imekuwa kinyume.
Kwa ujumla, kama ilivyo hata kwa vyakula vingine, maziwa ni miongoni mwa vinywaji vinavyotakiwa kutumiwa kwa uangalifu na kwa usahihi, kinyume na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwetu kuwa maziwa hayana madhara yoyote kwa binadamu.  

Monday, August 27, 2012

MSIBA WA KANUMBA... VILIO UPYAAAA...


MSIBA wa aliyekuwa staa wa muvi za Kibongo, Steven Kanumba umeanza upya kwenye Kijiji cha Izigo, Muleba, Kagera baada ya mama mzazi wa marehemu, Flora Mtegoa kuupeleka msiba huo huko sanjari na mchanga wa kaburi la Dar.

Akizungumza kwa masikitiko  makubwa, mama wa Kanumba alisema tangu kifo cha mwanaye hakuwahi kupeleka msiba kijijini kwake kama mila na desturi zinavyotaka.
Aliongeza kuwa hiyo yote ilitokana na kukosa muda kwani licha ya mazishi, bado watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi walikuwa wakiendelea kumiminika nyumbani kwake kwa lengo la kumfariji.
Alisema kuwa alipofika Kagera, alipokelewa na umati wa waombolezaji na msiba ulianza upya, jambo ambalo hakulitarajia.
“Nilipofika kijijini nilipokelewa na ndugu, jamaa na marafiki, kwa kweli msiba ulianza upya. Sikutarajia, watu walilia na kuomboleza,” alisema mama Kanumba.
Akaongeza: “Kwa kweli kutokana na hali ilivyokuwa, hata mimi mwenyewe nilijikuta nalia sana. Nilihisi siku hiyo ndiyo mwanangu alifariki dunia rasmi kwa jinsi watu walivyokuwa wakiomboleza.
Akaongeza tena: “Ilibidi tufanye mambo ya mila na desturi za Wahaya zikiambatana na kuzika mchanga niliouchota kwenye kaburi la Dar (Kinondoni).
Mama Kanumba alisema anamshukuru Mungu walizika salama (mchanga) na kwamba muda si mrefu alitarajia kurejea jijini Dar kutoka kwenye msiba huo.
 “Namshukuru Mungu tumezika salama kwa kweli, mimi mwenyewe naendelea vizuri huku nikinywa dawa za Kihaya, nakaribia kurudi Dar hivi karibuni,” alisema mama Kanumba.
Steven Charles Kanumba alifariki dunia Aprili 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa madai ya kusukumwa na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anashikiliwa na vyombo vya dola.

MAGAZETI YA AUG 23-25 2012


.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.
.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...