Wednesday, March 7, 2012

WEMA NUSURA AUAWE...!!!!



Wema.

Mwanzo wa timbwili.

Timbwili likiendelea.

Gari lililoharibiwa.

Watu wakishuhudia timbwili hilo.


UBAYA, ubaya tu! Tukio lililomkuta Wema Isaac Sepetu la kunusurika kuuawa katika fumanizi lake na mume wa kigogo wa Ikulu, linasadifu maneno hayo....

WEMA APONEA CHUPUCHUPU
Wema ambaye maisha yake yamekuwa kama muvi, anadaiwa kuponea chupuchupu kuondolewa uhai baada ya gari lake kugongwa na gari la mwanamke anayedaiwa kuwa mtumishi wa Ikulu, nyuma kukiwa na madai kwamba ni yule anayelalamika kuporwa mume na staa huyo wa filamu za Kibongo.

NI MAENEO YA MWANAMBOKA
Kasheshe hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu ya Machi 5, mwaka huu, nje ya Pub ya Last Drop iliyopo Mwanamboka, Kinondoni, Dar es Salaam.

HABARI KAMILI
Muda mfupi baada ya tukio hilo, mapaparazi wetu walifika eneo la tukio ambapo walimsikia mwanamke huyo akifoka kuwa mumewe ndiye aliyemhonga gari na kumpangia nyumba.
Alisikika akirusha maneno akiwa ndani ya gari lake kuwa siku nyingi alikuwa akimuwinda Wema ili amshikishe adabu kwa kumchukulia mumewe, mpango ambao siku hiyo ulifanikiwa.

GARI NDIYO CHANZO CHA YOTE
Huku akiwa mbogo, mwanamama huyo aliendelea kudai kuwa akiwa nchini Uingereza alinunua magari mawili, moja analotembelea, alilomgonga nalo Wema aina ya Toyota Discover TD4 lenye namba za usajili T644 BVD na Toyota Lexus Harrier aliyohongwa Wema lenye namba za usajili T211BXR analotembelea staa huyo.

Alidai siku chache baadaye alishangaa kutoliona gari hilo nyumbani na alipomuuliza mumewe akamwambia liko gereji kwa Wachina.

“Niliamua kufanya uchunguzi mwenyewe, ndipo nikagundua alikuwa nalo huyu ma***a (tusi),” alisikika mwanamke huyo.

Alisema wakati anakatiza jijini kwenye misele yake, aliliona gari hilo limepaki kwenye Pub hiyo ndipo akaamua ‘kuliblock’ kwa mbele.

MASHUHUDA WANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo hilo wakati mwanamke huyo analizuia gari hilo, mama huyo alikuwa akilisukuma gari la Wema kwa kutumia la kwake akilenga kulitumbukiza mtaroni lakini zoezi hilo lilishindikana baada ya kuzuiwa na mti uliokuwa pembeni mwa barabara.

BASTOLA NJE NJE
Ilidaiwa kuwa, wakati hayo yakiendelea, mwanamke huyo alishuka kwenye gari lake akiwa na bastola ili apasue matairi au amtoe roho Wema.
Hata hivyo, kabla ya kutekeleza azma yake, Wema aliyekuwa ndani ya Pub hiyo alitoka nje na kuanza kujibizana kwa maneno mbofumbofu.

KWELI WEMA KAUZU!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baada ya tukio hilo, Wema aligeuka kauzu zaidi ya dagaa kwani muda wote alikuwa akimletea nyodo mwenye mume huku ajininadi kuwa uzuri ndiyo uliomfanya mume wake apagawe naye.

ULINZI WA KUTISHA
Baada ya hali kuwa mbaya, ilidaiwa kuwa mwanaume aliyekuwa na Wema aliomba msaada Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ambapo walifika ‘wajeda’, ndipo Wema akapata nguvu ya kufoka kuwa kuna mapaparazi wetu hivyo wazuiwe kupiga picha.

BARABARA YA KAWAWA
YAFUNGWA KWA MUDA
Kufuatia tafrani hiyo, Barabara ya Kawawa, Kinondoni ilifunga kwa foleni kutokana na umati kutanda eneo hilo hadi polisi walipofika na kuwatawanyisha.

MARAFIKI WA WEMA WATIMBA
Wakati hayo yakiendelea, marafiki wa Wema ambao ni mastaa wenzake walitimba ili kumpa sapoti akiwemo Snura Mushi, Amisuu Malik, Soud Ally na wengine kibao.

Hata hivyo, baadaye ‘gari la Wema’ lilichukuliwa na ‘breakdown’ na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni kwa ajili ya kuandikisha maelezo.

WEMA ANASEMAJE?
Juhudi za kuzungumza na Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani muda wote ilipopigwa,  hata alipofuatwa nyumbani kwake, geti lilikuwa limepigwa kufuli.

KUMBE!
Katika mahojiano, Wema alinukuliwa akisema kuwa gari hilo alinunuliwa na familia yake ikiwa ni pongezi baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Neseeb Abdul ‘Diamond’, lakini sasa mambo yamebadilika, kumbe ni mali ya mtu.

HII IMEKAAJE?
Habari za jijini zinadai kuwa mkasa aliokutana nao Wema ulichongwa na mashosti zake ambao amekuwa akiwaringishia kwa ‘shopping’ za Dubai hivyo kumsapoti mwanamke huyo kwa kumpa a-z kuhusu ratiba za mnyange huyo hivyo kumnasa kirahisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...