Tuesday, March 20, 2012

MASHINE YA KUINUA MATITI YATUA DAR


Mashauzi.
Nisha.

WACHINA wamezua kizaazaa kingine Bongo baada ya kuingiza mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala...

Saa kadhaa baada ya ishu hiyo kuripotiwa na moja litokalo kila siku nchini, mapaparazi wetu walifika katika saluni inayotoa huduma hiyo iitwayo Blue Palace, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam na kushuhudia wanawake waliotimba mahali hapo wakitaka kuhudumiwa.

MTAALAMU WA KICHINA
Ilifahamika kuwa saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve na meneja wake, Trust Mwembe ina mtaalamu wa Kichina aliyetajwa kwa jina la Ciisy Pang (23), ambaye ndiye anayetoa huduma hiyo.
Pamoja na gharama ya huduma hiyo kuwa kubwa kuanzia Sh.150,000 kwa kichwa, lakini bado idadi kubwa ya wanawake ilishuhudiwa ikifika mahali hapo kuulizia huduma bila kujali kiwango cha fedha.
Hata hivyo, gazeti hili lilipotaka kushuhudia kifaa kinachofanya kazi hiyo kiitwacho Beauty machine (mashine ya urembo), ilishindikana kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi siku ya Jumatatu pamoja na kwamba wateja walikuwa wa kumwaga.

ETI INAREJESHA HESHIMA KWENYE NDOA!
“Fedha ni nini mbele ya kurejesha heshima ndani ya ndoa? Hakuna kitu kinachonigombanisha na mista wangu kama kulegea matiti yangu baada ya kunyonyesha mtoto wetu wa kwanza. 

“Nahisi amepunguza upendo kwa ajili hiyo, lakini sasa nimepata mkombozi,” alisema mama mmoja aliyekutwa nje ya saluni hiyo Jumatatu wiki hii akiwa na wenzake.

“Asikudanganye mtu, matiti magumu yana mvuto wake, wanaume wengi hawapendi yaliyolegea kama uji, kwa taarifa yenu sasa mtatukoma, tutakuwa vigori,” alisema mwanamke mwingine aliyekuwa anasubiri huduma.

Ingawa alielezwa kwamba afike siku ya pili yake,  lakini aligoma na kuendelea kung’ang’ania eneo hilo akihitaji huduma hiyo.

MASHINE INAFANYAJE KAZI?
Ilifahamika kuwa, mashine hiyo ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli maalumu kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.

Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambayo huchukua wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.

“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer  za nywele.

“Baada ya kumlaza mteja kitandani, tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa mtaalamu huyo wa Kichina na kuongeza:

“Tunaiwasha mashine kwa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika.”

MASTAA WAENDA KWA SIRI
Wakati huo huo, habari za kuaminika zinadai kuwa baada ya kunyaka mchongo huo zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuripotiwa, baadhi ya mastaa wamekuwa wakiibuka saluni hapo kwa siri ili kupata huduma.

HOT POT ililizungumza na baadhi ya mastaa kama wana taarifa zozote kuhusu huduma hiyo ambapo kila mmoja alikuwa na lake la kusema:

JACQUELINE PENTZEL
 ‘JACK CHUZ’
“Kama itakuwa ni tiba asili ni bomba lakini kama material (vifaa) yanayotumika ni feki, lazima kutakuwa na madhara. Siwezi kuthubutu kukitumia hivi hivi.”

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’ (pichani)
“Mh! Tukiangalie kwa makini hicho kifaa jamani, tusije tukamkufuru Mungu bure kwa vitu ambavyo havina maana. Hapo lazima kutakuwa na madhara hata kama si ya moja kwa moja lakini kwa baadaye kuna madhara makubwa.”

SALMA JABU ‘NISHA’
“Naogopa kansa, lakini ngoja nikakifanyie uchunguzi kwanza nione kama hakina madhara, labda ninaweza kwenda ila kwa sasa, aku! Naogopa kupata maradhi ya kujitakia.”

BABY MADAHA
“Aaah! Sana tu, mambo ya urembo na mimi tena! Hata usiulize lazima niende tu, mambo mengine baadaye lakini urembo kwanza.”

KUNA MADHARA?
Kila kitu kina faida na na madhara yake ambapo kwa mujibu wa Dk. Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...