Friday, March 2, 2012

Binti wa miaka 10 ajifungua mtoto wa kiume: Ni baada ya kubakwa mara kwa mara na baba yake!!!



Msichana mwenye umri wa miaka10 nchini Mexico amezaa mtoto wa kiume

Mtoto huyo, alizaliwa kwa kupitia upasuaji inayojulikana kama Caesarian Section katika Hospitali ya Wanawake katika mji wa Puebla na sasa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.

Msichana huyo anaendelea vizuri kiafya na amesharejea nyumbani baada ya kujifungua, na anamtembelea mtoto wake hospitali kila siku.

Mwendesha mashtaka wa mji wa Puebla anafanya uchunguzi kumtafuta mwanaume aliyefanya ngono na msichana huyo, sababu hiyo inachukuliwa kama ni ubakaji kutokana na umri wa binti huyo.

Hii si mara ya kwanza kwa msichana mwenye umri mdogo sana kujifungua nchini Mexico.

Mwezi Agosti mwaka jana, msichana Amalia, aliyekuwa na umri wa miaka 11, alijifungua mtoto baada ya vyombo vya sheria kutomruhusu kutoa mimba (abortion) kutokana na sheria ya Mexico kutoruhusu utoaji mimba ikivuka miezi mitatu.

Amalia alipata mimba baada ya kubakwa mara kwa mara na baba yake wa kambo kuanzia wakati ana umri wa miaka 10.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...