Tuesday, March 20, 2012

MIDUME YAANZA KUJIUZA




AMA kweli dunia imekwisha! Kila kukicha Wabongo wanabuni mbinu mpya ya kujipatia mkate wa siku bila kujali kama ni halali au haramu ambapo baada ya kusikia habari za wanawake kufanya biashara haramu ya kuuza miili au ukahaba kwa muda mrefu, sasa wanaume nao wameingia kwenye mkondo huo...

Uchunguzi wa muda mrefu ulibaini kuwa katika klabu, kasino na sehemu nyingi za starehe jijini Dar es Salaam, kuna idadi kubwa ya wanaume wanaojiuza kwa mijimama ya mjini yenye ‘mihela’ yao.


ISHU NI KUWA NA MWILI WA MAZOEZI
Uchunguzi wetu ulibaini kuwa vijana wanaojihusisha na biashara hiyo ni wale walio fiti kwa mazoezi ya ‘gym’ au wababeba vitu vizito wanaosifika kwa kutunisha vifua.


YAJIPANGA KLABU
Katika utafiti huo, midume hiyo ilibambwa laivu ikiwa imejipanga kwenye kasino maarufu iliyopo maeneo ya ‘ushuani’ Upanga Mashariki, Dar es Salaam wakisubiri wateja.


Mwanzoni shuhuda wetu alidhani ni mabaunsa wa kasino hiyo, lakini alitolewa matongotongo na mmoja wa askari aliyekuwa na bunduki aliyevalia sare ambaye alimtonya kuwa vijana hao siyo sehemu ya ulinzi wa eneo hilo bali wako kwenye biashara hiyo.


“Siyo walinzi bwana, hao ni watu wako kwenye biashara ya kujiuza, kama upoupo utaona kinachoendelea,” alisema mlinzi huyo kwa shari la kutochorwa jina kwenye ukurasa huu.

MIDUME YATONGOZWA LAIVU
Katika hali ya kushangaza, ndani ya kasino hiyo inayochezesha kamari, walizama wanawake wawili kisha wakawafuata washikaji hao waliokuwa wamejibanza ukutani na kuanza kuwatongoza.


Hakupita muda mrefu, jamaa wawili waliondoka na wanawake hao waliotakata ambapo ‘shushushu’ wetu aliwashuhudia wakiingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo huku wakiwadekea mijimama hao.
Ilibidi kuchunguza wanakoelekea ambapo ililitonywa kuwa wanakwenda kuwapa ‘dozi’ na wakimaliza watarejea kwa ajili ya kujipatia wateja wengine.

MWINGINE ACHUKULIWA, 
MMOJA AREJEA
Haukupita muda mrefu ambapo alifika mwanamke wa makamo aliyetapakaa dhahabu shingoni, mikononi na miguuni ambapo alionesha ishara ya kumwita kijana mmoja, ndipo washikaji hao walipoanza kupigana vikumbo kumuwahi lakini alichagua mmoja akatimka naye kusikojulikana.
Wakati huyo akichukuliwa, mmoja wa wale walioondoka awali alirejea ‘kijiweni’ na kuendelea na biashara hiyo.

SEHEMU NYINGINE ZA STAREHE
Katika klabu na sehemu nyingine za starehe biashara hiyo kwa sasa imeshamiri kwani haina kificho.

WAMO WAKE WA VIGOGO
Kuna madai kuwa, baadhi ya wanawake wanaowachukua vijana hao ni wake wa vigogo (wanasiasa) na watumishi wa serikalini ambao ndoa zao hazijatulia. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...