Saturday, March 24, 2012

Haijawahi kutokea; asiye na mikono,miguu...



Nicholas Vujicic ‘Nick’ (wa kwanza kulia) wakati wa harusi yake na Kanae Miyahara.
Nick akiwa na mpenzi wake Kanae. 

KIJANA Nicholas Vujicic ‘Nick’, hawezi kuisahau Februari 10, mwaka huu kwani ndiyo siku aliyofunga ndoa na msichana Kanae.
Siku ya ndoa yao, watu maalum walialikwa na baada ya hapo waalikwa walijichana kwa vinywaji na chakula baadaye maharusi hao wakaenda kufunga fungate Hawaii, Marekani.
Wazazi wa Nick, Dushka na mumewe Boris wenyeji wa Australia wanasema siku alipozaliwa mtoto wao huyo miaka 29 iliyopita walikata tamaa kama angeweza kuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, Mungu alimjaalia, akasoma na sasa ana shahada ya kwanza ya Mipango na Uhasibu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Griffith, Logan, Australia.
Anaweza kuandika kwenye kompyuta na anamudu kusugua meno yake kwa kutumia mdomo.
Jijini Logan, amefungua shirika lake lisilo la kiserikali la watu waishio bila mikono na miguu yeye akiwa afisa mtendaji mkuu (CEO) na ni mhubiri wa Neno la Mungu na amekwisha tembelea nchi zaidi ya 25 duniani. “Nimekuwa nikiwapa matumaini watu wenye ulemavu kwamba wanaweza kuishi maisha mazuri,” anasema Nick.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...