Tuesday, March 20, 2012

Ray, Lulu picha yao yazua utata...



Vincent Kigosi ‘Ray’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakiwa katika pozi la kimahaba. 

PICHA waliyopiga wasanii wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibu imezua utata kutokana na kupozi kimahaba huku kila mmoja akionekana kuwa na hisia kali kwa mwenzake.
Picha hiyo inayopatikana mtandaoni inamuonesha Lulu akiwa amevalia kigauni kifupi sana na macho yake yakiwa yamelegea huku Ray akiwa amemkumbatia kwa nyuma na mdomo wake ukiwa umeganda shingoni mwa ‘mtoto’ huyo.

Huku minong’ono ikienea kama moto wa kifuu kuwa wawili hao ‘wana-date’, Ray alitoa maelezo kupitia blogu yake kuwa picha hiyo waliipiga kwenye maandalizi ya filamu yake mpya inayotarajiwa kuwa sokoni muda wowote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...