Saturday, March 31, 2012

Mastaa wafanya pati ya ufuska


Baadhi ya mastaa waliotimba kwenye pati ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Kimwana Manywele 2006, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’ wanadaiwa kugeuza ukumbi kuwa uwanja wa ufuska kufuatia matukio machafu waliyoyafanya...

Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilichukua nafasi usiku wa kuamkia Alhamisi ya Machi 29, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sumit Kinondoni Mkwajuni jijini Dar ambapo mtangazaji huyo wa zamani wa C2C alikuwa akitimiza miaka kadhaa (aligoma kuitaja).

Awali, shughuli hiyo ilianza vizuri kwa ‘mtoto aliyezaliwa’ (Aunt Lulu) kuingia ukumbini akiwa amevalia kiheshima ambapo shampeni ilifunguliwa na wageni kula na kunywa huku wakimpongeza staa huyo.

‘SAPRAIZI’
Wakati pati hiyo inakaribia ukingoni, ghafla Miss Mara na Miss Tanzania 2001, Rashida Wanjara aliyeingia ukumbini hapo dakika kadhaa zilizopita alimmwagia Aunt Lulu ‘minoti’ ya elfu kumi kumi iliyokadiriwa kuwa zaidi Sh. laki 3.


MASHOGA WABADILI UPEPO
Wakati watu wakiendelea kutandika ulabu, ghafla vijana watano wanaodaiwa kuwa ni mashoga walianza kushindana kukata nyonga ukumbini humo, hali iliyofanya kila mtu kubaki kuwatazama wao.

MASTAA NAO WAHARIBU!
Mastaa waliofika ukumbini humo wakiongozwa na Isabella Mpanda, Rashida Wanjara, Aunt Lulu na wengine wengi walitia chumvi sherehe hiyo baada ya kucheza kihasara na kuacha maungo nyeti hadharani.

JINSI MOJA WADENDEKA
Pia baadhi ya warembo wanaojiita wadada wa mjini walipigwa chabo wakidendeka laivu wenyewe kwa wenyewe hivyo kusababisha pati hiyo kukumbushia enzi za Sodoma na Gomora kufuatia matukio hayo machafu.
Aunt Lulu ambaye siku hiyo alionekana mpole alidai kuwa, anajisikia vibaya kila siku kuandikwa akiwa na mavazi ya hasarahasara hivyo kuamua kubadilika kwa kutoka kitofauti siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...