Friday, March 2, 2012

MAHABA: MAMBO KUMI AMBAYO HUMUONDOLEA HAMU MWANAMKE NA KUKUONA KAMA MZIGO PINDI MNAPOKUWA PAMOJA, HATA KAMA ANAONYESHA ZAHIRI MBELE ZA WATU KUWA ANAKUPENDA…





1. UNYWAJI POMBE KUPINDUKIA

Unapokuwa Umetoka Na Marafiki Zako Wa Jinsia Moja Na Mko Kwenye Hafla Fulani, Au Ukawa Nyumbani Kwako Tu Peke Yako, Unaweza Kujisahau Na Kuzidisha Unywaji Wa Pombe.

Hili Ni Jambo La Kawaida Ambalo Huwatokea Wanywaji Wengi. Hata Hivyo, Kama Kweli Nia Yako Ni Kumpata Mwanamke, Au Kufanikiwa Kuzungumza Vema Na Mwanamke Uliyetoka Naye, Jiepushe Na Unywaji Wa Kupindukia. Wazoefu Wanasema Bia Moja Au Mbili Zinatosha Katika Muktadha Huu.

Kama Umekuwa Mzoefu Wa Kwenda Baa, Pengine Unafahamu Kuwa Wanawake Walio Makini Huwa Hawaitiki Miito Ya Wanaume Waliolewa, Bali Huwachukulia Tu Kuwa Ni Walevi Na
Kuwapuuza. Ni Wachuna Mabuzi Tu Ndio Huwachangamkia Wanaume Wa Aina Hii. Kwa Hakika, Kuwayawaya, Kuongea Kilevi Au Kuanguka Si Miongoni Mwa Sifa Azitakazo Mwanamke Kwa Mwanamume Na Ndiyo Maana Unapaswa Kuwa Makini Na Ulevi Unapokuwa Unamfukuzia Mwanamke.

2. UCHEZAJI MBAYA WA MUZIKI

Unapokwenda Kucheza Muziki Na Mwanamke Ambaye Umedhamiria Kumpata, Na Pengine Tayari
Umeshamweleza Nia Yako, Lazima Uwe Makini Na Uchezaji Wako. Mathalani, Zipo Nyimbo Ambazo Huruhusu Watu Kushikana, Hususan Blues, Lakini Si Ngwasuma Au Reggae.

Kujaribu Kumkumbatia Mlengwa Wako Katika Mapigo Ambayo Si Sawa, Au Kinyume Kabisa Na Matakwa Yake, Kutakutokea Puani. Kama Mwanamke Wako Ni Yule Anayejiheshimu
Asingependa Kufanyiwa Vituko Vya Aina Hii Na Ndiyo Maana Utapaswa Kuwa Makini Unapocheza Naye.

3. KUWA NA “EARPHONE” MASIKIONI

Ni Jambo La Kawaida, Hususan Kwa Vijana, Kutembea Wakiwa Na Earphone Masikioni Mwao, Wakila Muziki Wao Taratibu, Huku Wakiwa Hawataki Kujihusisha Kabisa Na Mambo
Yanayoendelea Duniani. Kama Uko Peke Yako Ni Sawa, Lakini Hii Haitakusaidia Iwapo Umedhamiria Kuzungumza Na Msichana Kwa Minajili Ya Kujenga Uhusiano Naye.

Iwapo Muda Wote Utakuwa Na Vitu Masikioni Mwako, Ni Kama Kumwambia Msichana Aliye Mbele Yako Kuwa Muziki Huo Ni Muhimu Kuliko Yeye Na Kwamba Unapenda Zaidi Kuusikiliza Muziki Wako Kuliko Kuisikiliza Sauti Yake. Lakini Pia, Namna Hii Utakuwa Unajifanya Kuwa Wa Muhimu Zaidi.
Hii Si Hali Ambayo Msichana Yeyote Ataipenda. Hapa Msichana Unayeweza Kumpata Ni Yule Tu Ambaye Ana Malengo Yake Mengine, Si Mapenzi Ya
Kweli.

4. UTANI ULIOPITILIZA

Kwa Mtu Mcheshi Na Anayejua Kutania, Utani Mzuri Unaweza Kuchukuliwa Vizuri Tu Na
Mwanamke. Naam, Wanawake Huwapenda Wanaume Wenye Kufahamu Jinsi Ya Kuwatania Na
Kuwafanyia Tashtiti. Hata Hivyo, Ni Rahisi Sana Kuvuka Mstari Na Kulitia Tembo Maji,
Kiasi Cha Mwanamke Kukuchukulia Tofauti Kabisa Na Ulivyokusudia. Huwezi Kufahamu
Mwanamke Huyu Ana Kumbukumbu Gani Kuhusiana Na Jambo La Aina Hiyo Maishani Mwake.

Unapokutana Na Mwanamke Kwa Mara Ya Kwanza, Jitahidi Kuepuka Utani Unaoweza
Kutafsiriwa Kuwa Matusi. Jitahidi Tu Kuwa Mchangamfu Lakini Si Kuvuka Mpaka. Pia
Epuka Kuwaponda Watu Wengine Hata Kama Lengo Lako Ni Kumpandisha Chati Yeye.
Mathalani Unaweza Kumwambia, “Umemwona Yule Dada Na Makalio Yake Ya Kichina? Makalio
Ni Yako Bwana, Maana Ndiyo Halisi”. Hii Haifai. Kauli Za Aina Hii Zinaweza Kumfanya
Mwanamke Akuchukulie Kuwa Unapenda Sana Kuchagua, Unajiona Babu-Kubwa,
Unajipendekeza Au Ni Mshamba. Sifa Hizi Zote Hazitakusaidia Kumpata Mwanamke Huyu
Bali Kumpoteza.

5. KAULI ZISIZOFANYIWA TAFAKURI

Zipo Kauli Za Kumwingilia Msichana Ambazo Zinaweza Kukukosesha Bahati Ya Kumpata
Msichana Huyo, Kwa Kumfanya Apoteze Kabisa Hamu Nawe. Baadhi Ya Kauli Huonekana Za
Bei Rahisi Sana Machoni Pa Mwanamke. Mathalani Unapomwambia “Kwa Nini Usiwe
Unanitembelea Mara Kwa Mara?” Au “Ulijificha Wapi Kipindi Hiki Chote Cha Maisha
Yangu?” Utajionesha Kama Mtu Asiye Mbunifu Na Asiye Na Mahaba.

Lakini Mbaya Zaidi, Msichana Atagundua Kuwa Kauli Ya Aina Hiyo Umeitumia Muda Mfupi
Uliopita Kwa Msichana Mwingine Na Kwamba Utaitumia Tena Kesho Kwa Msichana Mwingine.
Njia Nzuri Zaidi Ya Kumwingia Mwanamke Ni Kuwa Halisi Na Kujenga Mazingira Ya
Kumfanya Apende Kuendelea Kuwa Pamoja Nawe, Kinyume Chake Utauzima Moto Wake.

6. MANUKATO MENGI KUPINDUKIA

Wanaume Wa Zama Hizi Nao Wanataka Kunukia Vizuri. Hili Ni Jambo Jema Na Pengine Ni
Mapinduzi Katika Hulka Ya Mwanamume. Naam, Manukato Ya Kawaida Ya Wastani Yanaweza
Kumvutia Mwanamke, Lakini Unapopitiliza Na Kuzidisha Manukato Unaweza Kumsababishia
Mwanamke Kushika Pua Yake. Unapotaka Kutoka Kwa Ajili Ya Kukutana Na Mwanamke, Tumia
Tu Manukato Kidogo Kwa Ajili Ya Kuondoa Harufu Yako Asilia Ya Mwili. Iwapo
Utajiogesha Manukato Ni Rahisi Sana Kulitia Tembo Maji.

7. KUTUKANA, KUJIAPIZA

Mdomo Mchafu Hautakusaidia Kumpata Mwanamke Kuwa Mpenzi Wako. Na Hapa Hauzungumziwi
Uchafu Wa Kutopiga Mswaki, Bali Kutukana Na Kujiapiza. Ni Kweli Kuwa Humtukani
Mlengwa Wako, Lakini Ataona Na Hatasisimuliwa Na Hali Hiyo.

Wapo Wanawake Ambao Wataongea Vibaya Kwenye Simu Au Watawatukana Wahudumu Ukiwa Nao,
Lakini Hii Haina Maana Kuwa Na Wewe Ujisahau Na Kufanya Hivyo. Kumbuka Ni Wewe
Unayemwaga Sera, Si Yeye. Mwanzoni Kwa Uhusiano, Ni Muhimu Sana Kuwa Muungwana.
Mdomo Mchafu Ni Dalili Ya Mtu Mwenye Tabia Mbaya. Hii Si Sifa Ya Kumvutia Mwanamke
Kuja Kuishi Na Wewe.

8. MARAFIKI WASIOFAA

Wapo Vijana Wa Kiume Ambao Hupenda Sana Urafiki Na Huwa Na Kundi La Marafiki Wa
Jinsia Yao. Wakiwa Nao Hujisahau Na Kufanya Mambo Ambayo Hawawezi Kuyafanya Katika
Hali Ya Kawaida, Ikiwa Ni Pamoja Na Kulewa Sana Au Kuvuta Sigara. Kama Umekwenda
Kwenye Kampani Hii Ukiwa Na Msichana Ambaye Ni Mlengwa Wako, Ni Rahisi Sana Kumvunja
Moyo.

Kwa Hakika, Kampani Huathiri Tabia Ya Mtu. Kama Ni Kampani Nzuri, Yamkini Na Yeye Ni
Mzuri, Lakini Kama Ni Kampani Mbaya Na Yeye Atakuwa Mbaya. Unaweza Ukaapa Kuwa
Mwanamke Hawezi Kukuondoa Katika Kampani Yako, Lakini Kwa Hakika Hapa Ni Suala La
Kuamua Kama Unampenda Mwanamke Huyu Au Kampani Yako. Jambo Moja Li Wazi: Kampani
Mbaya Itakukosesha Mwanamke Unayempenda.

9. HARUFU MBAYA MDOMONI

Yawezekana Kabisa Kuwa Uchezaji Wako Mbaya Wa Muziki Haukumwondolea Hamu Mwanamke,
Wala Manukato Yako Yaliyopindukia. Hata Hivyo, Kwa Harufu Mbaya Ya Mdomo Unaweza
Kujihakikishia Kuwa Utamfukuza Mwanamke Wako, Maana Hii Ni Sawa Na Dawa Ya Koili
Imfukuzavyo Mbu.

Kwa Ujumla, Usafi Wa Kinywa Ni Kitu Muhimu Sana Katika Suala Zima La Mapenzi. Meno
Yenye Mabaki Ya Chakula, Midomo Michafu Na Harufu Mbaya Mdomoni Ni Mambo Ambayo
Yatamfanya Mlengwa Wako Afunge Virago, Maana Atajiuliza Kama Hukujali Kusafisha
Kinywa Unapomfukuzia Itakuwaje Baadaye Ukishajihakikishia Kuwa Naye? Lakini Pia
Mwanamke Atajiuliza Kama Kinywa Chako Ambacho Kiko Mahala Panapoonekana Ni Kichafu,
Je Kwingine? Kuwa Makini.

10. KWENDA NA MTOTO

Kuna Nadharia Kwamba, Wanawake Huwapenda Wanaume Wenye Watoto. Ni Kweli Kuwa
Mwanamke Anapomwona Mwanamume Akiwa Amembeba Mtoto Huvutiwa Naye Na Kumwona Kama
Baba Mzuri, Japo Haina Maana Kuwa Atataka Kuzaa Naye Au Kuwa Na Uhusiano Naye
Kimapenzi. Kwa Kuufahamu Ukweli Huu Wa Asili, Unaweza Kuamua Kwenda Na Binti Yako
Mdogo Unapotoka Na Mwanamke Unayemhitaji.

Tatizo Ni Kwamba, Si Kila Mwanamke Atakupenda Kwa Hili. Kwa Hakika, Mwanamke
Akishajua Kuwa Una Mtoto Na Huishi Na Mama Yake Linaweza Kuwa Tatizo Jingine, Maana
Atafikiria Kuwa Pengine Wewe Si Mume/Mpenzi Mzuri, Au Hujakomaa. Pia Ataanza
Kumfikiria Mama Wa Mtoto Huyo. Lakini Pia, Kumbuka Si Wanawake Wote Wana Roho Ya
Kimama. Hivyo, Kama Unataka Kupata Bahati Ya Kuendelea Kukutana Naye Angalau Kwa
Siku Kadhaa, Mfiche Kwanza Suala La Mwanao, Kwani Kumshangaza Kwa Kwenda Na Mtoto
Kutamvunja Moyo.

YAPUKE MAMBO HAYA

Kama Kweli Una Haja Ya Kumpata Mwanamke Aliyeyavutia Macho Yako, Kuusisimua Mwili
Wako Na Kuitesa Akili Yako, Lazima Ufanye Kile Uwezalo Kuhakikisha Kuwa Unajiepusha
Na Mambo Ambayo Yanaweza Kukukosesha Bahati. Yapo Mambo Mengi, Lakini Angalau Kwa
Kuanzia Yazingatie Haya Nawe Utajiongezea Fursa Ya Kuibuka Kidedea Katika Suala
Hili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...