Friday, March 30, 2012

Mpasuo wa Maya wachochea ngono ukumbini...





Gauni alilokuwa amevaa msanii wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ kwenye sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie, liliwapa wakati mgumu baadhi ya wanaume kufuatia mpasuo ulioacha wazi asilimia kubwa ya paja lake.

Tukio hilo lilinaswa na paparazi wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya msanii huyo kutinga ukumbini hapo, minong’ono ilianza kufuatia nguo aliyokuwa amevaa.

Huku akiwa hana aibu, msanii huyo aliketi na kuliacha paja lake wazi, kitendo kilichowafanya baadhi ya wanaume kuanza kumtolea maneno makali wengine wakidai anawashawishi ngono.

“Ndiyo nini sasa kutuvalia vile kama siyo kutuweka majaribuni tu?” alisikika akiwaka kijana mmoja aliyekuwa amekaa nyuma ya msanii huyo.

Hata hivyo, licha ya Maya kubaini kuwa, vazi lake lilikuwa likishawishi ngono aliendelea kupozi kimitego, kitendo kilicholaaniwa na baadhi ya watu waliomuona.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...