Saturday, March 3, 2012

BINTI AGOMBEA MWANAUME BAA...



Binti ambaye umri wake unakadiriwa kuwa kati ya miaka 15-16, aliyefahamika kwa jina moja la Fatuma, amezua sekeseke la aina yake akidaiwa kugombea mwanaume.
Tukio hilo la aibu na kusikitisha lilitokea Februari 29, mwaka huu, saa nane mchana ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar.
Awali, Fatuma alionekana akiwa ameketi na mashosti zake wakipata ofa ya pombe kutoka kwa mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Peter ambapo baada ya muda alitokea demu mwingine na kwenda kukaa meza nyingine.
Ilidaiwa kuwa, yule msichana aliyetinga ukumbini pale alikuwa ni mpenzi wa Peter hivyo katika kuua soo, mwanaume huyo alimtuma mhudumu awapelekee fedha Fatuma na wenzake na kumtaka akawaambie wasimfuatefuate tena.
Baada ya Fatuma ambaye muda mwingi alikuwa akijua kuwa ndiye atakayeondoka na Peter kwa madai ni mzuri kuliko wenzake kuhisi anataka kuachwa solemba, alinyanyuka na kwenda kumletea ‘vagi’ yule demu aliyewatibulia.
Aidha, kibinti hicho kilimporomoshea matusi mazito Peter akimwambia eti anashobokea mademu wenye mititi makubwa wakati kigoli (yeye) yupo.
“Wewe nilikuona mjanja kumbe hauna lolote, mjinga na fala mkubwa wewe,” alisikika akibwatuka binti huyo.
Maneno hayo yaliamsha hasira kwa Peter ambaye alinyanyuka na kuanza kumshushia kipigo Fatuma kiasi cha kuzua timbwili zito na kujaza watu.
Hata hivyo, baadhi ya wasamaria wema waliokuwa eneo hilo waliingilia kati na kumuokoa binti huyo akiwa nyang’anyang’a kwa kipigo.
Akizungumza nje ya ukumbi huo, binti huyo alisema: “Mimi namshangaa sana yule kaka, kunipiga bila sababu za msingi, kama ni ofa sijamuomba, amenipa mwenyewe, kwa nini anipige?” alihoji Fatuma huku akiondoka eneo hilo akiwa amenyong’onyea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...