Tuesday, December 6, 2011

Twanga Pepeta wafanya kweli Birmingham


Bendi ya Twanga pepeta ilifanya makamuzi ya nguvu katika mji wa Birmingham siku ya Jumamosi tarehe 3 Desemba 2011 ndani ya ukumbi wa La Reference iliyohudhuriwa na mamia ya wadau mbalimbali wa muziki kutoka pande zote karibu na mji wa Birmingham na vitongoji vyake pamoja na london. 

Wakati huo huo, Twanga wanatarajiwa kurejea nchini kesho alfajiri baada ya kumaliza ziara yao nchini Uingereza.

Tunapenda kutoa shukrani kwa wale wote walioweza kufika katika show hii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...