Friday, December 23, 2011

Mastaa waliotia Aibu 2011




Zimesalia siku 14 mwaka 2011 ufike ukingoni huku ukiwa umeacha aibu kwa baadhi ya mastaa wa Bongo...
Wema Isaac Sepetu anafungua dimba kwamba, mwaka 2011 ulikuwa wa misukosuko mingi kwake ikiwa ni pamoja na kupandishwa kortini ikiwa ni madai ya kumtusi msanii wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ (pichani).
Aidha, alikabiliwa na changamoto za kubwagwa na mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’. Hata hivyo, uhusiano wao bado upo kwenye gogoro.
DIAMOND
Kwake ulikwenda sawa, lakini ilipofika suala la kumvisha pete ya uchumba Wema, siku chache mbele kutangaza kummwaga kisha kumrudia kulimchafua.
BOB JUNIOR
Mwaka wa 2011 haukuwa mzuri kwa msanii huyo, kwani aliingia katika tifu zito na Wema. Bob Junior alimshtaki Wema kutokana na kumtukana matusi ya nguoni, chanzo kikiwa ni bifu lililokuwa kati yake na Diamond. Kesi hiyo iliishia katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni ambapo Wema alilipa  faini ya Sh.40,000.
JOKATE MWEGELO
Yeye anaufunga mwaka kwa aibu kufuatia zile tuhuma za hivi karibuni kutoka kwa Wema kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na jamaa yake, Diamond. Hata hivyo, Jokate alikanusha vikali madai hayo.
IRENE UWOYA
Huyu alitoa kali ya mwaka baada ya kutangaza kuachana na mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ huku akitoa maneno ‘mbofumbofu’ kuwa, hajawahi kumpenda tangu walipooana mwaka 2009.
Hata hivyo, Uwoya alishamalizana na mumewe kwa kumwomba msamaha baada ya kugundua kosa lake.
JACQUELINE PENTZEL
Ilikuwa aibu yake pale alipokuwa akisakwa na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar, akituhumiwa kumtusi mwandishi wa habari (jina linahifadhiwa). Kusakwa huko kulimnyima amani na kushindwa kujitokeza hadharani mpaka alipoamua kuomba msamaha, akasamehewa na kuwa huru.
VINCENT KIGOSI ‘RAY’ NA STEVEN KANUMBA
Hawa ni nyota wa filamu za Kibongo ambao awali walikuwa marafiki wa kupindukia, lakini walitia aibu baada ya kuingia kwenye bifu zito chanzo kikiwa ni kutambiana kuhusu magari yao ya kifahari waliyonunua wakishindana kwa kila mmoja kudai lake la gharama kubwa.
Inadaiwa bifu lao bado linaendelea. Wakati huo huo, Kanumba ameshanaswa akigandana na demu usiku mwingi hali iliyozua utata.
JACQUELINE WOLPER
Ni mwanadada anayejiheshimu lakini kwa mwaka 2011 ameshaandikwa na vyombo vya habari kwa madai mbalimbali kama kutoka na Diamond, kuitwa mwongo na Lulu na kupigana na Shilole.
Hivi karibuni ameingia kwenye mgogoro wa kudaiwa ‘kumtongoza’ Diamond kwa kumtumia meseji achilia mbali juzikati kufurumushiwa madongo na wasanii wenzake, Wema Sepetu na Irene Uwoya.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Ndani ya mwaka huu unaoelekea ukingoni, Lulu ametia aibu kwa skendo mbalimbali ikiwemo ya kuchanwa na wembe akituhumiwa kukutwa na mume wa mtu pia kuhongwa nyumba na kigogo mmoja.
Aidha, Lulu anamaliza mwaka kwa aibu ya kulewa na kufanya vituko kwenye mikusanyiko ya wenzake achilia mbali lile la kupigwa marufuku kuingia kwenye kumbi za starehe kwa sababu ya umri wake kuwa mdogo.
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Huyu ndani ya mwaka huu amekabiliwa na aibu ya ulevi wa kupindukia pamoja na ugomvi wa kila mara. Ameshafunga mtaa kwa aibu pale alipomfuata mzazi mwenzake, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ akitaka mtoto wake akamlee mwenyewe.
SALMA JABU ‘NISHA’
Mwanadashosti huyu ndani ya mwaka huu alitia aibu ya mwaka pale alipoandikwa kuwa yeye ni msagaji. Aidha akatoka akidaiwa kuwa mlevi wa kupindukia na uvutaji wa sigara.

AUNT EZEKIEL
Aunt alikabiliwa na skendo ya kumpiga staa mwenzake wa sinema, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ kisha kuswekwa ndani kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar.

Juzikati amedaiwa kumkwapua mume wa mnenguaji wa Bendi ya African Stars, Fasha Joshua, sanjari na hilo ni kuhongwa gari aina ya Toyota Cresta. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...