Wednesday, December 14, 2011

King Majuto HOI


KOMEDIANI namba wani Bongo, Athuman Majuto ‘King Majuto’ yu hoi kitandani baada ya kufanyiwa upasuaji katika kiungo kimojawapo mwilini mwake.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mchekeshaji huyo alifanyiwa upasuaji katika Hosptali ya Jaha iliyopo Ilala Bungoni, Dar es Salaam hivi karibuni ambapo alilazwa zaidi ya wiki moja na kuruhusiwa Desemba 10, mwaka huu.

“Kwa sasa yupo nyumbani Vingunguti, Dar anaendelea na matibabu, japo amekuwa akilalamika maumivu makali kila kukicha, lakini tunaendelea kumuombea Mungu apone haraka,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu kilisema kuwa, mzee Majuto amekuwa akimlalamikia bosi wake (jina halikupatikana) kwa kusema kwamba imefikia hatua watu wa karibu wanamtafuta ili kumjulia hali, lakini bosi huyo hajafanya hivyo.

“Wakati nazungumza na King Majuto juzi, alinisikitisha sana baada ya kusema anapewa huduma mbovu na bosi wake anayesimamia kazi zake na atakapopona hataendelea naye na anaona bora arudi kwake Tanga,’ alisema ‘sosi’ huyo.

Tulipozungumza na King Majuto alikiri kufanyiwa upasuaji na hali yake inaendelea vizuri. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...