Thursday, December 15, 2011

Dume lingine lilozaa laonesha ‘laivu’ mtoto wake



London, Uingereza
Scott Moore, mwanaume mwingine Duniani kutajwa kubeba mimba ameonesha picha za kichanga chake katika mtandao mara baada ya kujifungua.

Scott, ambaye ni raia wa Uingereza aliyechukua jukumu la mwanamke la kubeba mimba alijifungua mwezi uliopita na kujinyakulia sifa ya kuwa mwanaume mwingine kuzaa duniani.

Aidha, Scott na mumewe Thomas, walizaliwa wakiwa na jinsia za kike wakafanyiwa upasuaji na kuwekewa homoni za kiume, walimkaribisha Duniani mtoto wao waliyempa jina la Miles Machi 9, 2010.
Mwanaume huyo ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 30 amemuonesha mtoto wake huyo hadharani mtandaoni baada ya kichanga hicho kutimiza umri wa mwezi mmoja.

Mtoto Miles ni wa kwanza kwa midume hiyo ambayo wakati wanazaliwa mmoja (Scott) alikuwa akiitwa Jessica na Thomas alikuwa akiitwa Laura na walifunga ndoa kisheria katika jiji la California, Marekani na wamekuwa wakiishi pamoja tangu 2007.

Imeelezwa kuwa Scott alitamani kuwa mwanaume akiwa na umri wa miaka saba na wazazi wake wakagharamia upasuaji wa kuondoa matiti hata hivyo, wakashindwa kumgharamia uondoaji wa jinsia yake ya kike ambayo iliachwa bila kuondolewa.
Naye Thomas alitamani kuwa mwanaume akiwa na umri wa miaka mine lakini alipofikisha miaka 19 akabadilisha jinsia yake ya kike ambapo madaktari walichukua sehemu ya mwili wake kwenye paja na kumtengenezea uume.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...