Wednesday, February 29, 2012

MWINGIRA AKIRI KUNUNUA CHANGU


Nabii Josephat Mwingira.

ANAYEJIITA Mtume na Nabii, Josephat Elias Mwingira wa Kanisa la Efatha la jijini Dar es Salaam ambalo anadai ni la mwisho tayari kwa unyakuo,  amekiri kununua  changudoa ‘changu’ Mererani,  mkoani Arusha.

Mwingira amekiri hilo katika kitabu chake alichokiandika na kukisambaza sehemu mbalimbali  nchini kikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wito Wangu na Kusudio Langu’ ambapo amesema alibobea kwa kufanya zinaa na machangudoa.

Katika kitabu hicho chenye kurasa 34, Mwingira amesema licha ya uzinzi alibobea pia katika ulevi na kwamba siku moja akiwa na kahaba (Changu) huko Mererani Arusha alitokewa na Bwana Yesu ambaye alimuambia aachane na mambo hayo na amfuate yeye ili amtumikie.

Hata hivyo, Mwingira amesema licha ya wito huo wa Yesu, wakati huo alikuwa kwenye mazingira ambayo hayakuwa mazuri kwa sababu  alikuwa katika hali ya ulevi na mshiriki wa mambo mengi ya kidunia.

CHANGU ALITIMUA
“Yule dada (Changu) alipoona hali hiyo, akakimbia nikabaki peke yangu. Bwana Yesu akasema, mimi ninakutaka wewe uache maovu yote na unitumikie,” amesema Mwingira.
 Ameongeza kuwa baadaye wakati Yesu alipotaka kuondoka ikabidi amshike miguu na kumng’ang’ania na akamuambia,  “Usiniache!”.

Alifafanua kuwa Yesu akamshika bega la mkono wa kulia akasema, “Nitakuwa na wewe”, halafu akatoweka na baada ya hapo ndipo alipoanza kuombea watu.
Mwingira amekiri kuwa hata baada ya ‘kumuona’ Yesu, aliendelea kunywa pombe lakini ikawa anaitapika na akawa anatokewa na Kristo ndotoni au anatuma Malaika na kumuelekeza watu ambao atakwenda kuwaombea uponyaji kutokana na matatizo yao.

MCHUNGAJI AMPINGA
Hata hivyo, mchungaji mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa alipokisoma kitabu hicho alipingana na Mwingira, akasema Yesu hawezi kumtokea mtu akiwa katika harakati za kufanya ukahaba.

“Mungu anachukia sana ukahaba na mifano ipo. Aliteketeza Sodoma na Gomora ikawa jivu kutokana na watu wa kule kuendekeza ukahaba, aliunguza mji wa Babeli kutokana na mambo hayohayo, sasa siyo rahisi mtu atokewe na Yesu wakati yupo katika harakati za uhakaba,” alisema mchungaji huyo.
Aliongeza: “Mtu anaweza kutokewa na shetani la ngono kama atakuwa anaendekeza mambo hayo na baadaye kuwa moto kwelikweli wa uzinzi, hivyo kila mtu achukue tahadhari.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...