Wednesday, February 1, 2012

DIAMOND: NIMEMFUMANIA WEMA MPAKA NIMECHOKA! !!





Diamond.

Wema.

Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ amefyatuka mambo makubwa juu ya uhusiano wake wa kimapenzi na Wema Isaac Sepetu...


Akizungumza katika mahojiano maalum, Mwenge-Bamaga, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita, Diamond alisema kwa muda mrefu amekuwa mkimya akikwepa kuzungumzia uhusiano wake na Wema, lakini sasa ni zamu yake.


‘Kichaa’ huyo wa Bongo Fleva alisema kuwa, katika kipindi cha takribani mwaka mmoja alichodumu kwenye ‘malavu’ na Wema, amejifunza na kushuhudia matukio ya kutisha ya usaliti katika mapenzi yanayomhusu Miss Tanzania huyo wa 2006, mengi yakiwa ni mafumanizi yasiyohesabika.
“Unajua mwanzoni sikupenda kuweka hadharani mambo ya aibu ya Wema kwa sababu nilishatahadharishwa nikajifanya kichwa ngumu nikiamini angebadilika.


MAFUMANIZI KIBAO
“Nikianza na suala la kumfumania kila kukicha akisaliti penzi letu kwa wanaume wengine, nilishamfumania Wema mpaka nikachoka.
“Listi ya wanaume wa Wema ni ndefu, lakini fumanizi kiboko ni lile nililomkuta kitandani kama alivyozaliwa akifanya …(kitu kibaya) na rafiki yangu…(staa wa filamu za Kibongo),” alisema Diamond ambapo mahojiano yaliendelea hivi;
Utamu: Baada ya kumfumania ulichukua hatua gani?
Diamond: Nilimvuta pembeni nikampa kisago, aliniomba msamaha yakaisha, lakini bado aliendelea na mabwana zake.
Utamu: Unapomzungumzia Wema unaonekana una hasira, mbali na kumfumania amekufanyia nini kingine?
Diamond: Kinachoniuma ni kitendo cha kunitangaza kuwa ameniacha wakati mimi ndiyo nimemuacha.
Utamu: Ina maana mmeachana jumla?
Diamond: Usiseme mmeachana, sema umemuacha jumla? Kusema kweli mimi na Wema yamekwisha, simtaki na wala hakuna tena mapenzi.


YUKO TAYARI KURUDIANA NA WEMA?
Utamu: Je, Wema akikuomba mrudiane uko tayari?
Diamond: Siyo kwamba akiniomba, ameshakuja nyumbani na watu kibao kuniomba msamaha na akalala kwangu, nilimwambia awaombe radhi mashabiki wangu kwa kunichafua ‘then’ sitakuwa na kinyongo moyoni mwangu, nitamsamehe kama binadamu lakini sijui kama tutashirikiana tena mambo ya chumbani.
Utamu: Kwani alipokuja kwako kukuomba msamaha akalala, hamkushiriki mambo ya chumbani?
Diamond: Acha tu, nisingependa kuzungumzia kilichotokea usiku ule, lakini kulipokucha tu, alikuja kuchukuliwa akaondoka zake.


PETE YA UCHUMBA
Utamu: Umesema uhusiano wenu wa kimapenzi umefika kikomo, vipi kuhusu hatma ya pete ya uchumba ya shilingi milioni 3.6 uliyomvisha pale New Maisha Club Masaki, Dar mwaka jana kwani kuna taarifa kuwa ameshaivua?
Diamond: Sihitaji hiyo pete na sitamuuliza, kama mapenzi yamekwisha ataendelea kuvaa ya nini? Acha avue itamsaidia kupunguza ‘stress’.


FUMANIZI NA JOKATE
Utamu: Je, ni kweli kwamba alikufumania na Jokate (Mwegelo)?
Diamond: Namheshimu sana Jokate, sijui ningeanzia wapi kumtongoza. Aisee, asikwambie mtu, Wema alimchafua mtoto wa watu bila sababu yoyote na wivu wake wa kimapenzi. Hakuna kitu Jokate anachojuta kama kukubali kufanya video yangu kwani tukio moja tu, lilimharibia vibaya ‘future’ yake.


TUZO ZA MUZIKI MWAKA JANA
Katika hatua nyingine, Diamond alidai kuwa Wema ndiye aliyesababisha akakosa tuzo za muziki za Kili mwaka jana kufuatia skendo zilizokuwa zikimwandama hivyo mashabiki na wadau kumpotezea.
Alisema: “Wema alidai yeye ndiyo aliyenipaisha, lakini ukweli ni kwamba Wema alinitongoza kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kupata tuzo tatu za Kili mwaka juzi ‘so’ si kweli kwamba yeye ndiyo kanibeba, alinikuta nikiwa juu vibaya mno.”
Utamu ilimtafuta Wema kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake juu ya salata hili bila mafanikio.


KUTOKA Utamu
Tunafanya jitihada za kuwakutanisha Diamond na Wema laivu ili kumaliza mzozo uliopo kati yao hivyo usikose kufuatilia...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...