Wednesday, February 1, 2012

JIKE DUME LATIKISA JIJI... ANA NYETI 2, MOJA YA KIKE NYINGINE YA KIUME...



Mary katika pozi tofauti.

MWANAMKE wa aina yake aliye na viungo vya kike na kiume, amekuwa gumzo ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Mwanamke huyo anayeitwa Mary (25),  amekiri kwa kinywa chake kuwa ana viungo vyote vya kike na kiume na vinapiga mzigo sawia.
Awali, mapaparazi wetu waliinyaka ishu hiyo kutoka kwa rafiki wa karibu na Mary ‘Jikedume’ mwenye maskani yake Kimara, Dar ambapo alieleza kuwa mbali na ile ya kike, pia mrembo huyo ana nyeti ya kiume na mara nyingi marafiki zake wengi ni wanaume.

Ili kupata undani wa taarifa hiyo iliyozagaa jijini kama moto wa kifuu, mwishoni mwa wiki iliyopita, UTAMU iliamua kumsaka kwa udi na uvumba ambapo lilikutana na Mary maeneo ya Kinondoni, Dar anapopiga mzigo katika ofisi moja akitumikia nafasi ya katibu muhtasi, hivyo akaanika maisha yake ya kimapenzi akikiri kuwa alizaliwa katika hali hiyo na ameizoea.

YA KIUME NI ZAIDI
Mary alisema kuwa anaona ni kitu cha kawaida lakini mara nyingi huwa yenye nguvu na hisia zaidi ni ile ya kiume.

Mrembo huyo alisema kwa upande wa ile ya kike inafanya kazi kama wanawake wengine na ili kuweka mambo sawa, huwa ana mpenzi wake mmoja anayemtimizia mahitaji yake.

NI VIGUMU KUAMINI
“Najua ni vigumu kuamini, lakini kwa upande wangu, mimi najiona kawaida tu na namshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye aliyeniumba hivi, hivyo namrudishia sifa na utukufu, sijawahi kujuta kwani nitakuwa namkosoa muumba wangu,” alisema Mary.

Aliendelea kutambaa na mistari kuwa tangu alipozaliwa hakulelewa na wazazi wa kumzaa bali alikulia kwa shangazi yake jijini Mwanza, lakini alivyoendelea kukua, walezi wake walikuwa wanamuogopa kutokana na hali yake.

Alisema walezi wake hao walikuwa wakitafuta jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kumpeleka hospitali akatolewe jinsia ya kiume.
“Kabla ya kufanikisha zoezi hilo, mimi nilikimbia nikaja Dar kwa kuogopa labda wangenikamata wanikate kinguvu,” alisema.

ANATAKA CHA KIUME KIONDOLEWE
Alisema baada ya kutimba Dar, alisaka kazi ya kumpatia mkate wa siku na sasa amepata mfadhili atakayemsaidia kumpeleka hospitali kwa ajili ya kuondoa kiungo cha kiume kwa sababu anatamani siku moja aolewe.

Hata hivyo, Mary alisema mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Francis wapo kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wakiendelea kupeana mapenzi kama kawaida na ameridhika na hali yake.

Alisema endapo ikitokea kiungo cha kiume kinahitaji kufanya kazi, mpenzi wake huyo humchua hadi anarejea katika hali ya kawaida.
“Nikiamua naweza kumridhisha hata mwanamke, lakini huwa sitaki kuwa karibu nao,” alisema Mary na kuongeza:

“Napenda sana kampani ya wanaume, sina rafiki mwanamke hata mmoja. Pia akitokea mwanaume ananitongoza na mimi simtaki tunakubaliana, lakini tukifika huko ndiyo nambadilikia, hivyo wanaume wengi wananiogopa kutokana na hali niliyonayo.

“Nimezaliwa hivi, wanaume wengi wananiogopa na kuniona natisha au naweza kuwafanyizia.”

USHUHUDA
Kwa upande wake jamaa aliyewahi ‘kumtokea’ mwanadada huyo na kukubaliana kila kitu, ikashindikana kutoka na hali hiyo aliyetambulika kwa jina moja la Malick, kuwa anachokisema Mary, yeye alikishuhudia kwa macho yake hivyo ni kweli kwa asilimia zote.

Malick alikiri mwili kumwishia ganzi baada ya kuiona hali ya mrembo huyo na kuamua kutoka nduki.
“Tulikubaliana vizuri lakini siku ya kufanya tendo, ndipo niliposhtuka kuona ana viungo viwili hivyo nikatoka nduki kwa kuogopa na hadi leo huwa namuogopa,” alisema Malick.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...